HABARI MPYA

6/recent/ticker-posts

WAFUGAJI WA NYUKI WATAKIWA KUEPUKA MIGOGORO KWENYE SHUGHULI ZAO


Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (A/INSP) Omary Tembeleni.

Polisi Kata ya Lupalilo, wilayani Makete, mikoani Njombe,Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (A/INSP) Omary Tembeleni, amefanya mazungumzo na wananchi wa Kijiji cha Lupalilo wanaojishughulisha na shughuli za ufugaji wa nyuki na kuwasihi kuepuka migogoro katika utendaji wao wa kazi.

Tembeleni amesisitiza kuwa migogoro ya mipaka ya maeneo ya mizinga, umiliki, au tofauti za kimaslahi inarudisha nyuma maendeleo na inaweza kusababisha uvunjifu wa amani. 

Hivyo amewataka kutatua changamoto zao kwa njia ya amani na kupitia kwenye uongozi wao.

Jeshi la Polisi linaendelea kuimarisha ulinzi shirikishi ili kuhakikisha shughuli za kiuchumi za wananchi zinafanyika katika mazingira salama na yenye utulivu.

Post a Comment

0 Comments