![]() |
| Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Makete mkoani Njombe, Mrakibu msaidizi wa Polisi ASP Rehani Abuu akishiriki uzinduzi wa mradi wa nyumba ya kulala wageni katika Kata Iwawa wilayani humo |
Na mwandishi wetu - NJOMBE
Katika kuonesha matokeo chanya ya ushirikiano bora baina ya Jeshi la Polisi na wananchi kwenye kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu kupitia Polisi Jamii, Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Makete mkoani Njombe, Mrakibu msaidizi wa Polisi ASP Rehani Abuu ameshiriki zoezi la uzinduzi wa mradi wa nyumba ya kulala wageni katika Kata Iwawa wilayani humo.
Akizungumza ASP Abuu ameeleza uamuzi wa mmiliki wa nyumba hiyo kualika Jeshi la Polisi kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo ni kielelezo muhimu cha kuonesha namna ambavyo wananchi katika Wilaya hiyo wameelewa ipasavyo dhana ya Polisi Jamii katika kukuza mashirikiano kati ya Polisi na wananchi katika masuala ya mbalimbali na kuwa pongeza kwa juhudi hizo na kuwataka wawe mabalozi wazuri kwa ushirikiano huo kwa wananchi wengine.
Amebainisha kuwa, Jeshi la Polisi kupitia Kamisheni ya Polisi Jamii imeweka mikakati madhubuti inayolenga kukuza mahusiano na ukaribu kwa wananchi ili waweze kusaidia kukabiliana na vitendo vya uhalifu.
Faidon Kyando, ambaye ni mmiliki wa nyumba hiyo ameeleza kuwa ameshawishika kutoa kipaumbele kwa kiongozi wa Jeshi la Polisi kuzindua mradi huo kutokana na kutambua mchango na juhudi kubwa zinazofanywa Polisi wilayani humo kushirikiana na wananchi katika kulinda usalama wa raia na mali zao.


0 Comments