Na Essau Kalukubila.
KIKUNDI cha watu wenye ulemavu kilichopo Kiuyu Minungwini Wilaya ya Wete Mkoa Kisiwani pemba wametoa kilio C hao kwa serikali wakiiomba kuwapatia eneo la kufanyia kazi ili waweze kutimiza ndoto zao za kufungua kiwanda na kutoa ajira kwa vijana wengi .
Akizungumuza na mwandishi wa habari hizi Katija Mbarock ambae ni mwanzilishi wa kikundi hicho chenye watu 32 wakiwemo wenye ulamavu amesema wanafanyakazi katika mazingira mgumu kwa kukosa eneo lakufanyia kazi zao za ushonaji na ufumaji wa mashuka.
Aidha ameongeza kuwa licha ya viongozi kupita katika kikundi hicho nakuona changamoto zinazowwkabali lakini bado swala la eneo halijapatiwa ufumbuzi .
“Tumekuwa tukipokea watu wengi na viongozi mbalimbali vyama na serikali na kuwaeleza kwa kina changamoto zetu lakini bado wameshindwa kutatuliwa changamoto hiy"alisema .
Aliongeza "Waziri wa ofisi ya makamu wa kwanza wa rais Zanzibar Mh Harus Said Suleiman tulimweleza shida zetu akatulipia mlango wa biashara muda wa mwaka mmoja na kuahidi kututafutia eneo ili tuweze kutekeleza majukumu yetu na kutumiza malengo yetu” alisema Katija.
Mmoja wa wana kikundi hicho Aisha Hamad Said mtu mwenye ulemavu wa uziwi amesema amekuwa akijifunza kushona na kufuma mashuka na sasa ameona furaha katika kutimiza ndoto ya kuwa mshonaji mkubwa .
Hata hivyo amewaomba wadau mbalimbali kuwaona kwa jicho la huruma ili waweza kutimiza ndoto zao za kufungua kiwandi ili waweza kutoa ajira ningi kwa vijana wengi Zaidi.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar Mh Harusi Said Suleman abae pia ni mwakilishi wajimbo la Wete amesema tayari wapo kwenye mchakato wa kuwatafutia eneo kujenga kitega uchumi ili waweze kutimiza malengo Yao.
Ameongeza kuwa licha ya kuwa tunapambana kutafuta eneo lingine lakini wakati huu wanaendelea kutafutia ofisi ya kukaa kufanya kazi kwa uhuru katika maeneo ya chamanangwe.
“Ni kweli kikundi kile nakifahamu kwa sababu wana vijana wanapambana licha ya hali walizonazo na kwa kipindi hiki nipo napambana kuhakikisha wanapata ofsi katika viwanja vya chamanangwe".alisema.
Ikumbukwe kuwa kikundi cha UKOMBOZI WTU kilianzishwa mwaka 2020 kikiwa na wanachama 32 lengo likiwa Ni kuwakutanisha watu wenye ulemavu na wasio na ulemavu .
0 Comments