| Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, ACP Mahamod Banga |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, ACP Mahamoud Banga amewashukuru wananchi wa mkoa huo kwa kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika mazoezi ya pamoja kupitia POLISI NJOMBE JOGGING inayowaleta pamoja wananchi na askari wa vyombo hivyo mkoani humo.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa mazoezi hayo yanayofanyika kila siku za jumamosi, ACP Banga ameeleza kuwa mwitikio wa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki mazoezi hayo unaonesha ni kwa kiasi gani wananchi na vyombo hivyo vinaendelea kukuza mahusiano katika kulinda na kudumisha umoja na amani mkoani humo.
Kwa upande wake Kassim Mdotta ambaye ni mtaalamu wa mazoezi ya viungo, amewataka wananchi ambao bado hawashiriki mazoezi, kujitokeza kwa wingi zaidi ili kuimarisha afya ya mwili na akili kwani mazoezi hayo ni endelevu.
0 Comments