Na mwandishi wetu
Polisi kata za Bulongwa, Kipagalo na Luwumbu wilayani Makete, mkoani Njombe, mkaguzi wa Polisi, INSP Marwa Kisyeri amewatahadharisha wananchi kuacha tabia ya kupanda vyombo vya moto vilivyotengwa kwa ajili ya usafirishaji wa mizigo, ili kuepusha madhara na ajali zinazoweza kuepukika.
Ametoa rai hiyo wakati akizungumza na kutoa elimu ya usalama barabarani kwa abiria waliokutwa wamepanda kwenye chombo cha moto aina ya guta, pamoja na dereva wa chombo hicho.
![]() |
| Polisi kata za Bulongwa, Kipagalo na Luwumbu wilayani Makete, mkoani Njombe, mkaguzi wa Polisi, INSP Marwa Kisyeri akizungumza na abiria waliokuwa kwenye guta. |
Mkaguzi Kisyeri ameeleza kuwa vyombo vya mizigo havina mifumo au miundo ya usalama inayomkinga abiria pindi ajali au dharura inapotokea, jambo linaloweka maisha yao hatarini.
Aidha, amemtaka dereva wa guta hilo pamoja na madereva wengine wilayani humo kuzingatia kwa umakini sheria na kanuni zote za usalama barabarani ili kuepusha ajali na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya dereva yeyote atakayebainika kukiuka sheria kwa kubeba abiria kwenye vyombo vya mizigo.

.jpeg)
0 Comments