HABARI MPYA

6/recent/ticker-posts

WANANCHI WASHUKURU POLISI KATA KWA KUSAIDIA ELIMU KUTOJICHUKULIA SHERIA MKONONI

Polisi kata ya Luponde wilayani Njombe, mkaguzi msaidizi wa Polisi A/INSP Huruma Mwampashi akitoa elimu kwa wananchi.

Na mwandishi wetu

Polisi kata ya Luponde wilayani Njombe, mkaguzi msaidizi wa Polisi A/INSP Huruma Mwampashi, amewataka wakazi wa kata hiyo kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi pale wanapokumbana na changamoto au kutokea uhalifu katika maeneo yao na badala yake kuwasilisha changamoto hizo kwenye uongozi ili kuzitafutia ufumbuzi wa kisheria.

Ametoa rai hiyo wakati akitoa elimu kwenye kikao cha ushirikishaji jamii katika kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu kwa wananchi katika mtaa wa Madogo kwenye kata hiyo.

A/INSP Mwampashi ameeleza kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mkononi kama vile kujinyonga na kunywa sumu pale wanapokabiliana na changamoto mbalimbali jambo ambalo linaathiri usitawi wa jamii na taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi kupitia polisi jamii, linatekeleza mkakati wa ulinzi shirikishi ambao unalenga kuwaweka wananchi karibu na jeshi hilo kushirikiana kutatua changamoto mbalimbali za uhalifu ikiwa ni pamoja na kubaini, kuzuia na kutanzua vitendo hivyo vinavyorudisha nyuma maendeleo ya wananchi kwenye maeneo yao.

Hivyo amewaasa kutumia fursa ya uwepo wa polisi jamii kushirikisha changamoto zao kwa watu wao wa karibu au Polisi kata ili kuweza kutatua changamoto kabla ya kuchukua maamuzi ambayo ni kinyume cha sheria.

Inno Silvester Mligo, mwananchi wa kata hiyo amelishukuru Jeshi la Polisi kupitia Polisi jamii kwa kuwapatia mbinu na elimu mbalimbali za kushirikiana na jeshi hilo katika kukabiliana na uhalifu ambapo uwepo wa polisi kata umewasaidia kutekeleza majukumu yao kwa amani bila wasiwasi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Luponde, Erasto Japhet Mwabena amebainisha, elimu inayotolewa na polisi jamii imesaidia kupungua kwa vifo vitokanavyo na kujichukulia sheria mkononi katika kata hiyo kutoka matukio saba hadi tukio moja kwa mwaka jambo ambalo linaonesha matokeo chanya ya elimu zinazotolewa na polisi kata.

Post a Comment

0 Comments