HABARI MPYA

6/recent/ticker-posts

JAMII YAHIMIZWA KUFUFUA VIKUNDI VYA ULINZI SHIRIKISHI

Na mwandishi wetu

Jamii katika Wilaya ya Wanging'ombe imetakiwa kuimarisha na kuboresha vikundi vya ulinzi shirikishi ili kudhibiti matendo ya kiuhalifu na kuimarisha amani katika maeneo yao.


Wito huo umetolewa na Polisi Kata ya Igwachanya, Mkaguzi wa Polisi, INSP Saidi Mataru, wakati akizungumza na kutoa elimu ya usalama kwa wananchi wa Mitaa ya Mtapa na Chalowe iliyopo ndani ya kata hiyo.


INSP Mataru amesisitiza kuwa ulinzi na usalama unaanzia ngazi ya jamii, hivyo kushirikiana kwa karibu na vyombo vya dola kupitia vikundi hivyo kutasaidia kubaini na kuzuia wahalifu mapema kabla hawajaleta madhara.

Ameeleza, "Ulinzi shirikishi ni nguzo kuu ya amani katika mitaa yetu. Tunapokuwa na vikundi thabiti vinavyofanya kazi kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi, tunafanya maeneo yetu kuwa magumu kwa wahalifu kujificha. Kila mwananchi ana wajibu wa kuwa mlinzi wa mwenzake."

Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wameushukuru uongozi wa Jeshi la Polisi kupitia polisi kata kwa elimu hiyo na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kufufua na kuwezesha vikundi hivyo vya ulinzi shirikishi ili kulinda usalama wa mali na maisha yao.

Post a Comment

0 Comments