Na mwandishi wetu
Washiriki wa mazoezi ya pamoja baina ya vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Njombe kupitia POLISI NJOMBE JOGGING wamepatiwa elimu ya unyonyeshaji kutoka kwa mtaalamu wa lishe, Beartha Nyigu ikiwa ni sehemu ya utoaji wa elimu kuhusu umuhimu wa maziwa kwa mtoto katika mwendelezo wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama.
Aidha Kamanda wa Polisi mkoa huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Mahamoud Banga amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi katika mazoezi hayo yanayofanyika kila jumamosi ikiwa ni pamoja na kuambatana na watoto wao ili kuwajengea afya bora kupitia mazoezi hayo.
"Tunataka watoto wetu wakawe mabalozi wa wenzao kwamba Jeshi la Polisi ni rafiki wa watoto. Jogging hii ni endelevu, kwa hiyo kila jumamosi tukutane kuendeleza jogging yetu ili kuboresha afya zetu," Ameeleza ACP Banga.
0 Comments