Na Essau Klaukubila.
Chama cha wandishi wa habari wanawake Tazania TAMWA Zanzibar kisiwani Pemba wamezitaka asasi za kiraia na tasisi za Serekali kutowa ushirikiano katika kutekeleza mradi wa Mabadiliko ya Tabia nchi.
kauli
hio imetolewa na Meneja wa Mradi wa ZANZADPT Zoni ya Pemba Ali
Hamad wakati alipokuwa akitowa utambulisho wa mradi kwa asasi za kiraiya na
tasisi za Serekali katika ofis za SHIJUWAZA Chake Chake Pemba.
Amesema katika mradi huo wa kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi
yamekuja kuwakomboa wanawake Katika nyanja mbali ikiweo kiuchumi na kuweza
kupaza sauti katika kutetea haki zao.
Wakati huo huo Nairat Abdullah Ali Afisa Program kutoka TAMWA_Zanzibar
amesema Kila mmoja anajukumu la kuchukuwa hatua ya kukabiliana na mabadiliko ya
Tabianchi hasa Kwa kutumza mazingira kwakupanda Miti Ili kukabiliana na
mabadiliko hayo ambayo yamekuwepo Kwa kiasi kikubwa.
Nae Juma Bakari Alawi mratibu AZASPO Pemba ameipongeza TAMWA
Zanzibar kwa kushirikiana na washirika wa Mradi huo kwa kuchukua jitihada
za kuazisha mradi huu, utasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabiayanchi,
kwani Kuna maeneo mengi yameanzaa kupotea uhalisia wake hususan katika
maeneo ya baharini.
Haji Nassor Mohd kwa niamba ya wandishi wezake wameomba
Jumuiya ya Wandishi wa Habari Wanawake TAMWA Zanzibari
kuwashirikisha watu wenye mahataji malum wakati wautekelezaji wa Mradi huo ili
kuweza kukabiliana na Mabadiliko ya Tabiya ya nchi.
Amesema ipo haja ya kutolewa elimu kwa mwalim ToT kwani wamesema
hawakuwashirikisha watu mwenye mahitaji malum kutokana hali zao jambo ambalo
litapelekeya kuwakosesha haki ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabiaya ya nchi.
Jumuiya ya Uhifadhi wa Msitu Pemba CFP inautambulisha mradi
wa ZANZADPT kwa wadau kisiwani Pemba na kuelezwa kuwa asilimia 80
wanufaika ni wanawake.
0 Comments