HABARI MPYA

6/recent/ticker-posts

SHEHA WA KWANZA WA KIKE ZANZIBAR AIFANYA KOANI KITOVU CHA MAENDELEO.

 


Na Thuwaiba Habibu.

Mpaka miaka  ya karibuni  hakuna aliyetarajia  atatokea mwanamke kuwa sheha, lakini  kama usemi wa Waswahili  unavyosema  mambo kangaja huenda  yakaja.

Kwa uchaguzi wa wawakilishi wa serikali mitaani na vijijini wanaojulikana kama masheha ambao siku zote ulikuwa kwa wanaume sasa kilichokuwa kinangojewa kimekuja.

Nacho ni kwa mwanamke kushika nafasi hii.

Aliyefungua mlango na kuweka historia hii ni Bi Tunza Ali Shaali kuwa sheha wa kwanza katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Mlango aliofungua umeipelekea idadi ya masheha wa kike kuongezea kama takwimu inavyosema mpaka Sasa masheha wa kike  79 ikiwa jumla ya sheha wote ni 388 na wanaume wakiwa 309 licha ya kuwa Bado Kuna asilimia ndogo za washeha hao lakini muamko unaonekana kuwepo kuliko hapo awali.

Bi Tunza, sasa akiwa na miaka 63  alichaguliwa kuwa sheha wa Koani, nje kidogo ya mji wa Unguja, mwaka 2002 .

Wakati masheha wengi huduma kwa kipindi kisichozidi miaka 10 bibi huyu ameendelea kushika wadhifa huo kwa a miaka 21 sasa.

Bibi huyu alichukua nafasi hio muda mfupi tu baada ya aliyekuwa sheha wa kijiji hicho, Bwana  Omari khamis, kuiaga dunia.

Alisema  alipochaguliwa kuwa sheha na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini  unguja bwana Mustafa Mohd Ibrahim

Hii ilitokana na kutoamini na zaidi kwa vile hakuwahi kusikia kuwepo sheha wa kike.

Aliamua kupiga Moyo konde na kukubali nafasi hii na kukubali kubeba jukumu hilo kwa kuamini alikuwa na uwezo wa kuiongoza jamii inayomzunguka.

"Kwanza nilikataa uteuzi hu, lakini mwalimu wangu wa chuoni ambaye pia alishawahi kuwa mkuu wa wilaya, Mzee Muhammed Zubeir,  alinihamasisha kwa kuniambia  naiweza kazi hii na na mimi nikaridhia kutokana na hamasa nilioipata", alieleza.

Bi Tunza ndio alifanya fika za wanawake kuelewa kuwa

Kama tunavyojuwa safari ya uongozi kwa mwanamke siku zote huwa sio nyepesi kwa vile huwa na kupitia njia mbovu, yenye milima na mabonde  na kona hatarishi.

Lakini licha ya ugumu huo wanawake wengi wanapambana na kuonyesha uwezo mkubwa wa kufikia malengo  na ndoto zao.

Kwa upande wake, Bi Tunza amekuwa anahakikisha maendeleo yanapatikana katika shehiya yake kwa kushirikiana na watu anawowaongoza.

Alisema alianzisha kamati za maendeleo ili kusimamia shughuli za kimaendeleo katika shehiya hio.

Jambo la kwanza alilolifanyika kazi  ni kujenga skuli kwa sababu watoto wa shehia hio walikuwa wanakwenda mbali kufuata elimu, kutoka Koani adi Kidimni.

Hivi sasa shehia hii ina skuli za maandalizi na msingi na imekuwa na matokeo mazuri katika mitihani.

Vile vile alihakikisha kuwa kilimo kinakuwa vizuri katika shehiya yake kwa kuboresha mabonde ya kilimo ya kibonde maji ambayo sas yanazalisha mazao mbali mbal, hasa  matunda na mboga mboga.

Ukosefu wa maji safi na salama ya uhakika kulininyima amani na alihangaika sana hadi wakafanikiwa  kupata huduma hii .kutokana na juhudi zake watu wa shehia yake walifanikisha kupata maji ya uhakika na salama.

Kabla ya hapo walikuwa  wakichota maji katika mtoni na kwenye visima vya kuvuta .

Alisema katika shehia ya Koani nyumba ziliokuwa na umemem zilikuwa zinaheshabika, lakini yeye na kamati yake walihakikisha umeme unafika hadi Koani na sasa nyumba nyingi zinatumia nishati hii.

Maendeleo yote haya yametokana na  kwa kuwa karibu na wananchi wenziwe na kamati alizoziunda kwa lengo la kuleta tija ndani ya eneo lake.

Kama tujuavyo kwenye mafanikio hakukosi changamoto. Miongoni mwa matatizo aliyokumbana nayo ni dharau  na baadhi ya watu  kutompa mashirikiano    katika shughuli za kimaendeleo.Hii ilitokana na wengi kuona harakati za maendeleo kwa njia za kujitolea katika shehia nyingi zinazoongozwa na wanaume hazikuoata mafanikio.

Changamoto nyengine  ambayo inamuumiza kichwa bi Tunza ni kukoseana kwa barabara za ndani katika maeneo ya Kibonde Maji, sehemu ambayo inatumika kwa kusafirisha mazao.

Hatua ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya kutoa nafasi za uongozi kwa wanawake inakwenda sambamba na maelekezo y mkataba wa kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni wa 1966.

Katika Ibara ya 3 ya mkataba huu, nchi ziliotia saini mkataba zimezitaka nchi wanachama, Tanzania ikiwemo, kuhahikisha uwepo wa haki sawa kwa wanawake na wanaume katika kupata haki zote za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

Bi Tunza ni mwanamke ambaye anahamasisha wanawake wenziwe kuingia katika uongozi ili kuenda sambamba viongozi na waume  katika kuiletea Zanzibar maendeleo.

Hivi sasa anatoa elimu kwa akina  mama katika vikundi vya ushirika na kuwahamasisha kugombania uongozi  kwa kuwafundisha njia na mikakati ya kugombea nafasi mbali mbali za uongozi

Alisema kabla ya kuwa sheha alikuwa ni mwananchi wa kawaida aliyekuwa na mashirikiano mazuri na kila mtu na  mwenye kuheshimu wakubwa na wadogo na anaamini hio ndio sababu iliyopelekea ateuliwe kuwa sheha.

Mkulima mmoja wa shehia ya Koani, Bi Fatma Othman Khamis, ameueleza uongozi wa Bi Tunza kuwa ni mzuri na linalofurahisha ni kwamba wanapolalamikia jambo wanaona juhudi za kulitatua zinafanyika.

Alisema wakulima wanamshukuru sheha wao kwa kuhakikisha serikali imewaletea makandarasi wa kuwatengenezea miundo mbinu ya  kumwagilia  maji ambayo iliwasaidia, ijapokuwa sio kwa kiwango wanachokitarajia

Mwalimu mkuu wa Skuli ya Koani Shaibu Ali anamueleze  Bi Tuna kama kiongozi mwenye mashirikiano makubwa na amehakikisha wamepata uzio wa skuli ili kuepusha uharibifu wa rasilimali na kupunguza utoro wa wanafunzi.

Nao wananchi wa koani walimueleza Bi Tunza ni  mama wa shehiya ya Koani anyeibeba shehia yake vizuri

Alitoa mfano wa juhudi anaofanya zakupambania na  kuwepo vijana wanaotumia dawa ya kulevya na kupeleka nguvu kazi za eneo hilo kupotea.

Wananchi wengi wanamsifia Bi Tunza kwa tabia nzuri na kushirikiana nao katika maendeleo na maelezi ya watoto .

Uongozi mzuri wa huyu mama katika shehiaya Koani ni kielelezoi chengine cha uwezo wa mwanamke kuongoza kwa uadilifu na umahiri,.

Mpe nafasi mwanamke aonyeshe uwezo wake wa kuongoza.

mwisho

Post a Comment

0 Comments