Na Thuwaiba Habibu.
Kwa muda mrefu wamekuwepo watu wanaoamini uongozi unahitaji nguvu za misuli na kutokana na misuli ya mwanamke kuwa dhaifu kuliko ya mwanamume sio busara kukabidhi uongozi kwa mwanamke.
Watu hawa hawaelewi kwamba uongozi ni
kuonyesha watu njia nzuri, bali wapo wengine wanaoweza kuwapeleka wengine
katika safari yao kwa usalama na uhakika.
Miongoni mwa hawa
wanawake, wengine wakiwa dhaifu sana kwa umbo, lakini wenye nguvu na
umahiri mkubwa wa kuongoza wenzao kujipatia mafanikio.
Upo ushahidi wa kutosha, tokea dahari
na enzi, wa waanawake shupavu na majasiri walioongoza jamii kupata maendeleo na
hata kupata ushindi katika vita.
Kwa bahati mbaya bado wapo watu
katika jamii yetu na nyingi za wenzetu wanaona uongozi ukishikwa na mwanamke
basi hakuna cha maana kitachofanyika.
Hii ni kwa sababu wamejijengea dhana,
kuamini na kuwataka watu wengine kuwa kama wao kwa kuwa mwanamke ni dhaifu
kimwili basi pia ni dhaifu, hana uwezo wala maarifa au ubunifu unayohitajika kuweza kuongoza
wenzake.
Haya
ni zaidi ya lile la kuona
mwanamke ni mtu wa kufikiriwa kipi afananye na apewe au kusikilizwa anasema
nini na sio muhimu wakati mwengine kutilia maanani maoni yao, hata yakiwa ni
umuhmu.
Hi ndio iliyopelekea mwanamke kuwa na
nafasi ndogo ya kujielezea katika
jamii na ndio maana hii leo pamekuwepo
na muamko mkubwa wa wanawake kujitokeza kuonyesha uwezo na ujuzi wao wa
kuongoza.
Katika harakati hizi wanawake
wanaopigania haki yao ya kuongoza wamepambana na kila aina ya vikwazo, ikiwa
pamoja na kuambiwa wanaingia eneo wasilostahiki kuwepo.
Pamoja na haya ni kejeli, unyanyasaji
wa kila aina, maneno yasifaa na kukashifiwa wao na familia zao kwa lengo la
kuwakatisha tamaa na kuwarudisha nyuma.
Wao wamekuwa wakuambiwa ni wakuzaa na kulea watoto ,na kuwachukulia
kama mapambo ndani ya nyumba zao tu. Wanaume wengine huwachukulia kama ni
chombo tu Cha starehe zao.
Lakinibaadayabaadhiyawanawakekupatiwaelimu
juu ya uongozi na njia za kukiuka vikwazo vinavyowakabili wapo waliochomoza sio
tu kuwa na uwezo, bali wamefanikiwa na kuwa kigezo cha kupigiwa mfano mzuri wa
uongozi bora na wenye tija.
Elimu hiyo iliwafichua wanawake
waliokuwa tayari kutetea haki za wanawake na watoto wao na kuonesha kuwa mwanamke sio duni wa fikra kama
baadhi ya watu wanavyodhani.
Mbali ya ushahidi uliopo katika nchi
mbali mbali hapa kwetu pia wapo wanawake walioshika nyadhifa kubwa, jambo
ambalo katika miaka ya nyuma lilionekana kama ndoto ambayo si ya asubuhi,
mchana wala usiku.
Katika mwaka 1973, Rais wa Jamhuri ya
Muungano, Mwalimu Nyerere, alipomchagua mwanasheria Juliie Manning, sasa ana
miaka 82 kuwa Jaji wa kwanza wa Mahakama Kuu Tanzania na Afrika Mashariki na
Kati watu walishangaa na kuona kama jambo la ajabu. Wapo waliosema:Ilikuwaje?
Hawa watu walisahau au kufumbia macho
ukweli wa kuwepo wanawake, Bara na Visiwani, waliokuwa mstari wa mbele katika
harakati za kugombea uhuru na kuvumilia kila aina ya sulubu waliopata, kama
wenzao wanaume.
Kumbukumbu zinaeleza baadhi ya watu
walifika mahakamani kuona hicho ‘kioja’ cha kuwa na Jaji mwanamke katika
Mahakama Kuu ya Tanzania.
Jaji Manning alionyesha uwezo mkubwa
wa kusimamia na kutoa haki na hakutereshwa na mbwembwe na uzoefu wa wanasheria
wanaume wa ndani na nje ya nchi wakati akiendesha kesi.
Miaka miwili baadaye Jaji Maning
alichaguliwa Waziri wa Sheria na kushika wadhifa huo mpaka mwaka 1975.
Kati mmoja wa mihimili mitatu ya
nchi, Bunge, Tanzania ilipata Spika wa kwanza mwanamke, Mh. Anna Semamba Makinda, katika mwaka 2010 na
kuifanya kazi hio kwa uadilifu mkubwa mpaka 2015. Kabla ya hapo alikuwa Naibu
Spika.Mh. Makinda alisimamia sawia haki
za wanaume na wanawake ndani ya Bunge na pia alikuwa Kamishna wa zoezi la
kuhesabu watu (sense) liliofanyika mwezi Agosti mwaka jana.
Alipokuwa Spika, Mama Anna alihakikisha
wabunge wanafuata kanuni na taratibu huku akihimili kila aina ya vishindo ndani
ya chombo hiki cha kutunga sheria za nchi.
Mara kadha alilazimika kufanya
maamuzi magumu, kama kumtoa nje Mbunge aliyekiuka taratibu, kuonyesha ukaidi au
utovu wa nidhamu.
Hii inamaanisha kwamba alikuwa na
mamlaka ya kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wabunge ambao walikiuka kanuni
hizo.
"Pia maamuzi magumu ambayo
anaweza kuwa amefanya yanaweza kuwa ni pamoja na Mama Anna alisema alipokuwa
akifanya kazi ya Spika aliangalia sheria na kanuni na sio jinsia.
Kule Ujerumani, Kansela Angela Merkel
aliiongoza nchi hio na chama chake cha Christian Democratic Union kutoka mwaka 2005 hadi2021.
Akiwa mwanamke wa kwanza kuwa Kansela
wa Ujerumani alifanya maamuzi muhimu na magumu, ikiwa pamoja na kufungua
milango ya nchi yake kwa maelfu ya wakimbizi kutoka nchi mbali mbali katika
mwaka 2015.
Vile vile alikuwa na ushawishi mkubwa
katika siasa za Ulaya na dunia nzima na aliweka msisitizo mkubwa katika usawa
wa kijinsia na kuongeza uwakilishi wa wanawake katika uongozi wa serikali.
Katika serikali yake, aliunda baraza la
mawaziri lenye uwiano sawa wa kijinsia, ambalo lilikuwa hatua muhimu katika
kuhakikisha usawa wa kijinsia katika ngazi ya uongozi.
Merkel pia aliimarisha sheria za
kulinda haki za wanawake na kupambana na unyanyasaji wa kijinsia. Serikali yake
ilianzisha sheria kali dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia na udhalilishaji, ikiwa
ni pamoja na kuongeza adhabu kwa wanaofanya vitendo hivyo na kuweka mifumo bora
ya kutoa msaada na ulinzi kwa waathirika.
Hatua hizi zilikuwa muhimu katika
kuhakikisha usalama na ustawi wa wanawake nchini Ujerumani.
Hata huvyo Merkel alifanya jitihada
za kuwezesha wanawake kiuchumi na kijamii. Serikali yake ilianzisha sera na
mipango ya kukuza ushiriki wa wanawake katika soko la ajira.
Vile vile aliongeza fursa za elimu na
mafunzo kwa wanawake, akahamasisha usawa wa malipo kazini, na kuwezesha
upatikanaji wa huduma za utunzaji wa watoto. Hii ilikuwa hatua muhimu katika
kuhakikisha wanawake wanapata fursa sawa za kiuchumi na wanaweza kujitegemea
kifedha.
Ukiyaangalia haya niliyoyaeleza na
mengine hivyo kweli bado anaweza kutoea mtu kusema mwanamke hawezi kuogoza?
Tuangalie katika enzi za kiongozi wa
dini ya Kiislamu, Mtume Muhamma (SAW) ya
wetu Mtume tunaambiwa kwa usahihi kuwa sio tu alishirikiana na wanawake
katika uongozi, bali ia aliwapa nafasi ya kuongoza, hata katika mapigano ya
kusimamisha dini ya Kiislamu.
Vile vile alitoa umuhimu mkubwa
katika kusikiliza ushauri uliotolewa na wanawake.
Miongoni mwa wanawake walio shikilia
nyadhifa za umma au nyadhifa kubwa kubwa katika karne ya mwanzo na ya pili
Hijria, na kushirikiana na mtume ni hawa:
Mwanamke wa mwanzo aliyeshika na
kukubaliwa wadhifa wa ushauri kwa Mtume (SAW alikuwa mama yetu mkubwa,
Sayyidatuna Khadija binti Khuwayld (Radhiya llahu Anhu) ambaye alikuwa mshauri
wake mkuu kwa hali na mali.
Hata siku moja, Mtume (SAW) hakuwahi
kuukataa ushauri wake.
Mwanamke mwengine ni Bibi Rufayda
Al-Aslamiyya (Radhiya llahhu Anhu) ambaye alikuwa muuguzi
shupavu na jasiri na alikuwa akibeba silaha yake, na kujenga hema la
kuuguza majeruhi wa Kiislamu vitani.
Rafayda alishiriki vita mbali mbali vya Jihad,
miongoni mwao ni vita vya Uhud. Mtume alimuona akiwa amevaa jambia lake au jisu
lake, akamuuliza umevalia silaha hiyo kwa ajili gani? Rafiyda kamjibu: “Adui
yeyote ataye nisogelea nitapigana naye hadi
aniuwe au nimuuwe!” Mtume akatabasamu! .
Kwa bahati mbaya pamekuwepo na misemo
ambayo inayolenga kushusha hadhi ya
mwanamke na kumdogosha ndani ya jamii hata
kama ana uwezo mkubwa.
Misemo hiyo ni "Mwanamke Hana nguvu mbele ya mwanamme" . Hii inatokana na tafsiri
potofu ya kumtaka Mwnamume amsimamie mwanamke.
Huu usemi umetumwa kama kisingizio cha
kuwadumaza wanawake ili wasipate haki zao za kibinaadamu na za kiraia,. Huu ni
uonevu ambao jamii haipaswi kuupuzia au kuuvumilia.
Zawadi Madawili ni afisa mstaafu
mwanamke wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Madawili alikuwa mwanamke wa kwanza
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kuwa luteni toka mwaka 1975.Aliweza kuwa na
cheo cha brigedia mkuu mwaka 2003.
Madawili aliweza kuripotiwa katika
Mpango wa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa kuondoa athari za kiuchumi ndani ya
nchi na bara. Madawili pia aliweza kuanzisha jitihada zikizofanywa na uharakati
wake kuchochea hisia za wanawake wa Tanzania kuanzisha mpango wake.
Madawili alifikia cheo cha Meja
Jenerali kabla ya kustaafu.
Mnamo Oktoba mwaka 2017 alichaguliwa
kwenye bodi ya kuwezesha Huduma za Jamii ambayo ilikuwa imeanzishwa katika
kulipia watumishi wa umma
Yote hayo
aliweza kufanya hivyo baada ya kupata mafunzo ya kijeshi na kutokana na uzoefu wake wa miaka anaamini
wanawake wanao uwezo mkubwa wa uongozi.
Sio vizuri kwa wale wahafidhina
wanaoona shida kuwa na kiongozi mwanamke
kujifanya ni wagonjwa wa macho na hivyo hawana uwezo wa kuona wakati ipo
miwani ya kuwasaidia kuona vizuri.
Nayo ni hii mifano michache ya
wanawake viongozi tokea Dahari na enzi na hivi sasa niliyoielezea kwa
muhtasari.
Kinachohitajika ni kwa wanaume na
wanawake kushirikiana na kufanya kazi pamoja kwa maendeleo ya jamii na nchi
yetu.
Kama wasemavyo Waswahili…Mnyonge
mnyongeni, haki yake mpeni na wanawake nao wanastahili kupewa haki yao ya
kuongoza wenzao.
(Makala hii imeandalia na thuwaiba
kwa msaada wa mtandao)
0 Comments