HABARI MPYA

6/recent/ticker-posts

TAMWA ZNZ yatoa tuzo kwa Wnahabari Mahiri wa Habari za Takwimu kwa Wanawake na Uongozi 2022/223

Mshindi wa kwanza kipengele cha magazeti Hussna Mohamed Khamis akikabidhiwa tuzo na Waziri wa habari Zanzibar Tabia Maulid Mwita

·        Radio jamii na mitandao ya kijamii zang’ara

JUMLAya waandishi wa habari 10 wameibuka kidedea katika tuzo za umahiri za uandishi wa habari za takwimu za wanawake zilizoandaliwa na TAMWA, Zanzibar.

Miongoni mwa vipengele ambavyo vilikuwa vinashindaniwa ni pamoja na muandishi mahiri katika kipengele cha radio za kitaifa, radio za kijamii, magazeti pamoja na mitandao ya kijamii, ambapo kwa upande wa magazeti kulikuwa na washindi watatu, mitandao ya kijamii watatu, radio za kijamii washindi wawili na washindi wawili kutoka katika radio za kitaifa.

Katika washindi hao 10 waliopatikana, jumla ya washindi wane (4) wa kwanza kutoka katika kila kipengele walipatiwa zawadi ya cheki ya  milioni moja, tuzo pamoja na vyeti vya ushiriki.

Washindi hao wane kutoka katika kile kipengele ni pamoja na Husna Mohammed Khamis kutoka gazeti la Zanzibar Leo, Rehema Juma Mema kutoka radio Asalaam, Zuhura Juma Said wa mtandao ya kijamii wa Habari Portal na Amina Masoud Jabir kutoka radio Jamiii Mkoani kisiwani Pemba.

Washindi wa pili nao walijipatia vyeti pamoja na cheki ya tsh laki 5 kwa kila mmoja, ambapo mshindi wa tatu katika kila kipengelke alizawadiwa cheti pamoja na cheki ya shilingi laki nne.

Tuzo hizi za uandishi wa habari za takwimu kwa wanawake ni muhimu sana katika kushajihisha waandishi wa habari wa Zanzibar kuandika zaidi habari na makala kuhusiana na masuala ya wanawake na uongozi, lakini pia kutoa takwimu ya idadi sahihi ya wanawake walioko katika uongozi Zanzibar 

Zuhura Juma Saidi kutoka mtandao wa Pembaportal alieibuka mshindi wa tuzo ya wanahabari kupitia mtandao wa kijamii akikabidhiwa zawadi na katibu mtendaji wa Tume ya utangazaji Zanzibar Suleiman Abdalla.

TAMWA, Zanzibar imeamua kuchukua juhudi mahasusi za kuandaa tuzo hizo ili jamii itambue mchango wa wanawake na uongozi katika sekta mbalimbali ili kuinua hali za wanawake na kuongeza ushiriki wao  katika masuala ya uongozi ili kufikia 50 kwa 50 katika katika ngazi zote za maamuzi.

Mapema akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa TAMWA, Zanzibar Dkt Mzuri Issa aliiomba Serikali kuhakikisha kwamba ile asilimia 40 ya ushiriki wa wanawake ifike katika kila nyanja ya vyombo vya maamuzi ikiwemo kamati, bodi za utendaji.

Aidha, alisisita umuhimu wa kuandaa takwimu za wanawake na Uongozi itasaidia kujua hasa tuko wapi katika malengo hayo ambayo ni ya kimilenia Lengo la 5 la SDGs. Na sisi taasisi zetu tunaahidi kutoa mashirikiano ya kina.

TAMWA, Zanzibar inatoa wito kwa waandishi wa habari wa zanzibar kuendelea kuandika habari zinazohusu wanawake, takwimu lakini pia vikwazo mbalimbali vinavyomzuia asifikie nafasi za uongozi na kuwa tayari kushiriki katika tuzo zijazo ambazo zitaandaliwa.

Mgeni Rasmi katika hafla hiyo y tuzo alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae alisema kuwa Serikali imewasikia na tuko njiani kuzibadilisha ili muifanye kazi yenu kwa umahiri zaidi na bila ya wasiwasi wowote. Tunataka kuwa na sheria ambayo imetokana na pande mbili yaani wadau wa habari na Serikali.

“Nimekuwa nikifuatilia vyombo vya habari na kuona kuwa  Sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari, Magazeti na Vitabu namba 5 ya mwaka 1988 na marekebisho yake ya mwaka 1997 na  Sheria No.8 ya 1997 na marekebisho yake ya mwaka 2010 zikilalamikiwa zaidi kuwa na mapungufu na zinahitaji kurekebishwa pamoja na  sheria nyingine kadhaa zinazohusiana nazo”.

Tuzo hizo ambazo ni mara ya pili kutolewa zimeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ), kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO) na Ubalozi wa Norway.

Jumla ya kazi 421 kutoka vyombo vya habari vya aina zote vikiwemo magazeti, redio,  televisheni pamoja mitandao ya kijamii, zilipitiwa katika kutafuta washindi hao katika  tuzo hizo zenye kauli mbiu “KALAMU YANGU MCHANGO WANGU KWA WANAWAKE” hivyo waandaji wa tuzo hizo zinawaomba waandishi wa habari kujitahidi kuandika habari za kina za wanawake na uongozi.

Post a Comment

0 Comments