HABARI MPYA

6/recent/ticker-posts

KAMPENI YA USALIMISHWA WA HIARI WA SILAHA HARAMU YAZIDI KUTOLEWA NJOMBE


Wananchi wa Kijiji cha Igwachanya kilichopo Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe wamefikiwa na elimu kuhusu Kampeni ya Usalimishaji wa Hiari wa Silaha Haramu, huku wanaomiliki silaha hizo wakitakiwa kutumia fursa hii kuzisalimisha kwa hiari kwani hakuna hatua zitakazochukuliwa dhidi yao.

Elimu hiyo imetolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Wanging'ombe, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Justine Kamfulumbwe, akiwa ameambatana na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya hiyo, Mkaguzi wa Polisi INSP Eliminata Amani, wakati wa mkutano wa utoaji elimu na uelimishaji jamii uliofanyika kijijini hapo.


SSP Kamfulumbwe amewataka wananchi kutumia fursa hiyo kusalimisha silaha hizo haramu kwa hiari katika Vituo vya Polisi au Ofisi za Serikali za Mitaa bila hofu ya kuchukuliwa hatua za kisheria.


Katika hatua nyingine amewataka kuacha tabia ya kumaliza au kusuluhisha kesi za jinai mitaani na katika ngazi za familia kwa kusisitiza kuwa kuwa kesi za jinai hazipaswi kusuluhishwa kifamilia bali zifikishwe katika vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka.

Kwa upande wake, INSP Amani amewakumbusha wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao, hasa katika kipindi hiki wanachokuwa masomoni na pindi wanapokuwa likizo, ili kuwaepusha na makundi mabaya na kuwalinda dhidi ya vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji.


Wananchi wa Kijiji cha Igwachanya wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa elimu hiyo kuahidi kutoa ushirikiano katika kusalimisha silaha, kutoa taarifa za matukio ya jinai, na kulinda usalama wa watoto wao.

Post a Comment

0 Comments