Sheha wa Tumbatu Uvivini ndugu Ngwali Sheha Haji, amesema miongoni mwa changamoto zinazopelekea kutokuwepo ushiriki sawa wa kijinsia katika michezo ni pamoja na kukosekana kwa miundo mbinu rafiki na skuli kutokua na muda maalum wa michezo kwa wanafunzi.
Sheha
Ngwali amesisitiza kuwa mila na desturi sio kikwazo kwani historia inaonesha
kuwa kuna wanawake mbalimbali kutoka kisiwani hapo ambao wamewahi kushiriki
michezo na kuwa vinara katika kisiwa hicho.
“Hapo
zamani miaka ya 1973 wakati mimi ni mwanafunzi kulikuwepo wanawake wanaoshiriki
michezo na kuchukua medali nyingi lakini ushiriki umepungua kutokana na
changamoto za ukosefu wa mazingira rafiki ya kushiriki michezo kwa watoto wa
kike”, alisema Sheha Ngwali.
Nae
Mwalimu mkuu msaidizi skuli ya Tumbatu Msingi “A” ameeleza kuwa skuli hiyo ina
mikakati ya kuwahamasisha watoto wa kike kushiriki michezo hususan baada ya
kukamilika viwanja rafiki vya michezo kupitia mradi wa michezo kwa maendeleo
Kwa
upande wa wanafunzi wa kike wanaoshiriki michezo hasa mpira wa mikono (netball)
katika skuli hiyo wamesema kushiriki kwao katika michezo kumewasaidia
kuimarisha afya zao, kutembea sehemu mbalimbali pamoja na kupata zawadi.
Pia
wameiomba serikali na wadau mbali mbali kuwaunga mkono kwa kuwasaidia vifaa
mbalimbali vya michezo ikiwemo mipira, jezi na vyenginevyo ili iwe rahisi kwa
wao kushiriki katika michezo.
Katika
muendelezo wa utekelezaji wa mradi wa michezo kwa maendeleo, Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA ZNZ) kimefanya ziara
maalum pamoja na waandishi wa habari kutembelea kisiwa cha Tumbatu kuangalia
hali ya michezo katika kisiwa hicho.
Akizungumza
katika ziara hiyo mkuu wa kitengo cha mawasiliano TAMWA ZNZ Sophia Ngalapi
amesema kazi kubwa ya TAMWA ZNZ ni kutetea haki za wanawake na watoto pamoja na
kukuza usawa wa kijinsia katika kila sekta ndani ya jamii.
Ameeleza
kuwa lengo la ziara hiyo ni kuangalia hali ya kimichezo ndani ya kisiwa cha
Tumbatu ikiwemo ushirikishwaji wa jinsia zote katika michezo, miundo mbinu
pamoja na kupata maoni kutoka kwa wakaazi wa kisiwa hicho juu ya ushiriki wa
watotot wa kike katika michezo bila kuharibu mila, desturi na silka za
wazanzibari.
0 Comments