Na Essau kalukubila
KUKOSEKANA Kwa kiwanja cha mchezo wa volleyball katika Skuli ya Micheweni kumetajwa kukwamisha ndoto za watoto wakike kushindwa kufikia malengo yao.
Wakizungumza na mwandishi wahabari hizi kwa nyakati tofauti wanafunzi wa Skuli hiyo wamesema ndoto zao ni kuwa wachezaji wazuri wa mchezo huo ambao wataiweza kuiletea sifa nchi lakini kutokana na changamoto iliyopo imefifisha ndoto zao.
Hivyo wameiomba serikali kupitia wizara ya michezo kujenga kiwanja cha mchezo huo Ili wale wenye ndoto waweze kujifunza zaidi na kutimiza malengo yao.
Shakila Faki Juma mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Skuli ya sekondari Micheweni amesema kukosekana kwa kiwanja hicho kunapelekea kushindwa kuongeza ujuzi zaidi wa mchezo huo.
Naye mwalimu wa michezo wa Skuli hiyo Hamad Ali Hamad amesema kuwa watoto wa kike na wakiume wanania ya kufahamu mchezo wa volleyball na kucheza kwani wanapo kwennda kwenye mashindano ya kikanda wanafunzi huishia kutamani.
Kwa upande wake Afisa Elimu wilaya ya Micheweni Mwalimu Ismail Ali Hamad amekiri kuwepo kwa upungufu wa viwanja vya michezo hasa katika Skuli zilizopo wilaya hiyo.
Ameongeza kuwa licha ya kutokuwepo Kwa viwanja vya michezo hasa kiwanja cha volleyball lakini watoto wa kike wamekuwa wakishiriki kwenye michezo mengine Kama vile mpira wa miguu, Pete , kukimbia pamoja na michezo ya Sanaa.
0 Comments