HABARI MPYA

6/recent/ticker-posts

Kamati GEF: Jitihada zinahitajika zaidi kukuza Haki na Usawa wa Kiuchumi kwa Wanawake

ZANZIBAR 

KATIKA kufuatilia utekelezaji wa Programu ya Kizazi chenye Usawa, Kamati ya Kitaifa ya Ushauri kuhusu utekelezaji wa Programu hiyo imeanza ziara Zanzibar kwa kutembelea miradi mbalimbali ya uwezeshaji ikiwemo mradi wa Bear Foot uliopo Wilaya ya Kaskazini A, Unguja na Kituo cha kulea na kukuza wajasiriamali wabunifu (Incubation Centre) kilichopo Mbweni, Wilaya ya Magharibi B.

Katika kituo cha kulea wajasiriamali, kamati hiyo imesema jitihada zaidi zinahitajika kuwasaidia wanawake na wasichana kufikia lengo la Haki na Usawa wa kiuchumi kupitia shughuli za ujasiriamali kutokana na vikwazo wanavyokabiliana navyo.

Imeelezwa licha ya Zanzibar kuwa na wajasiriamali wengi wanawake lakini wengi hawajarasimisha biashara zao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa elimu ya umuhimu wa kurasmisha biashara pamoja na gharama za urasimishaji jambo linalopelekea kukosa fursa za kukua kiuchumi.

Mwenyekiti wa zaiara hiyo, Mhe.Mgeni Hassan Juma ambaye ni Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ameeleza.

 "Tuna kazi kubwa ya kuhakikisha tunawatoa wajasiriamali wetu kutoka katika uzalishaji wa chini hadi uzalishaji wa juu kwasababu rasirimali za kuwezesha kufanya hivyo tunazo."

Kwa upande wake Fatma Mohamed Juma, mkurugenzi Idara yuratibu wa Mafunzokituo cha kulea wajasiriamali, aliomba wadau kusaidia kuwekwa kwa mpango wa ufadhili wa ubunifu kwa wajasiriamali wadogo ili kuwahamasisha kubuni bidhaa mbalimbalim kwa ubora.

Alieleza wajasiriamali wengi wanashindwa kukua na kuzalisha bidhaa bora kwa kukosa mitaji ya kufanya ubunifu wa bidhaa mpya zenye kuendana na mahitaji ya masoko.

"Ili tuendelee lazima kuwepo na bajeti ya (ufadhili wa ubunifu) innovation fund ili kuwawezesha wanawake kubuni bidhaa kwa ubora, kwasababu kuna wanawake unakuta wanazalisha bidhaa nzuri lakini kutokana na uwezo wake mdogo anashimdwa kuendelea zaidi na ubunifu." Fatma Mohamed Juma, mkurugenz Idara ya uratibu wa Mafunzo, kituo cha kulea wajasiriamali.

Post a Comment

0 Comments