HABARI MPYA

6/recent/ticker-posts

Othman Masoud akutana na Askofu Kigoma


Kigoma

Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo taifa Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba chama hicho kinalenga kufikisha mawazo mbadala kwa watanzania kwa dhamira ya kuunga nuvu za pamoja ili kusaidia kujenga nchi kimaendeleo.

 Mhe. Othman ambaye pia ni makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameyasema hayo  alipokutana na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Kigoma Mhasham Josep R. Mlola ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Mkoani umu ikiwa ni maadhimisho ya chama hicho kutimia miaka kumi tanu kuanziswa kwake .

Amesema  kwamba  kufanya ivyo ndio kutekeleza ipasavyo kazi ya vyama vya siasa ambapo  msingi wake  mkuu ni kuunanisha kidemokrasia kwakuwa chama hico hakiamini kwamba siasa ni mapambano  bali kinaamini ni namna bora ya kuweza kuwafikia watu na kuweza kushaurinana kwa masirikiano juu ya namna bora ya kuleta mabadiliko .

Aidha amefaamisha kwamba msingi mwengine unaotumiwa na chama hicho ni  kuendeleza kukosoa kistaarabu kwani kufanya hivyo hakuhitaji lugha ya kukirihisha bali ni kujena usawishi kwa watu na kuweza kukubalika.

 Akizungunzia suala la Katiba Mpya Mhe. Othman amesema kwamba jambo hilo ni muhimu kuwepo chombo cha mawazo  shirikishi ambalo ni Bune lakini Bune lililopo sasa alina uwakilishi sahihi wa wananchi kutokana na kutokuwepo uchaguzi huru na wahaki.

Hata hivyo, amesema kwamba Viongozi na Taasisi za dini zinanafasi muhimu katika kujenga  Imani kwa wananchi na kuweza kufikia malengo yanayokusudiwa na taasisi za vyama vya siasa.

Akizununzia suala la Serikali ya Umoja wa Kitaifa Mhe. Othman amesema kwamba chama chake akioni furaha wala fahari ya kutananza kujitoa lakini kinalazimika kufanya ivyo kutokana na mazingira ya kutokuwepo dhamira ya kweli  kama masarti ya kuingia kwenye serikali hiyo jambo ambalo halikuwa rahisi.

Alisema kwamba Chama chake kipo tayari  na kinakaribisha ushauri na maelekezo kutoka kwa viongozi na taasisi za dini mbali mbali pale inapoonekana kwamba kuna mambo hayaendi vyema kwa nia ya kuleta umoja kwenye ujenzi wa nchi.

Naye Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma Mhasham Josep R. Mlola amekipongeza chama  hico kwa kuweza kujijenga na kusambaa nchi nzima katika kipindi kifupi cha miaka kumi tokea kuanziswa kwake.

Amekitaka kuendelea kujitaidi kuwa sauti ya wasionasauti kuwatetea watu wa Tanzania na kwamba ni muhimu kutumia mbinu ya mazungunzo katika kufikia vyema maleno na matarajio ya wananchi kupitia majukwaa ya siasa.

Mhe. Othman yupo Mkoani Kigoma kuendelea na ziara yake ya kuadimisa miaka kumi tokea kuanzishwa kwa chama hicho  na anatarajiwa kumaliza ziara yake katika Mkoa wa Tabora baadae wiki hii.

Post a Comment

0 Comments