Na Essau Kalukubila.
KATIKA kukuza uwezo wa watu wenye
ulemavu kiuchumi kumeanzishwa vikundi
vya kuweka na kukopa mabavyo vikundi hivi
vina idadi ya watu 30 kwa kila kikundi
kina watu (20) watu wenye ulemavu
na watu (10) ni watu wasio na ulemavu kwa lengo la kushilikiana.
Mafanikio haya ya kuanzisha vikundi
hivi imekuja katika mradi wa KIJALUBA ambao unatekelezwa kwa muda wa miaka 2
kwa ushirikino wa shirikisho la watu
wenye ulemavu (SHIJUWAZA) na Chama cha Wandishi wa Habari wanawake Tanzania, TAMWA
Zanzibar ambapo mradi huu ni wamajaribio
na unatakelezwa kwa kipindi cha
miaka miwili kwanzia mwaka 2022 hadi mwaka 2024
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi Bi Husina Hamadi Ali Mwenyekiti wa kikundi cha Tukiwezeshwa tunaweza
amesema tangu kuanzisha kwa vikundi hicho yeye amekuwa akipata faida nyingi ikiwemo ya kukusanyika kwa kubadirishana mawazo
na kupata pesa kwa njia ya kikundi kuweka na kukopa
Ameongeza kuwa kwamiezi iyayo kikundi
chao kitakuwa na faida kubwa kutokana na wanakikundi hicho kukipenda na kufuata mashariti ya kuweka na kukopa nakufanya kikundi hicho kusonga mbele
“matarajio yatu katika kikundi
nikukusanya pesa zikiwa nyingi tugawe ili tujiendeleze katika maisha yetu
ambayo tulikuwa tumekata tamaa lakini sasa mwanga umeanza kuonekana katika maisha
yetu kwakuanzishiwa kikundi hichi cha kuweka na kukopa” alisema Bi Husina
Shamkubwa Hamisi ni Mtu mwenye ulemavu
wa viungo na nimama mwenye watoto wawili
lakini yeye anasama flaraha imerejea kwake baada ya kuanzisha kikindi cha kuweka na kukopa ivisasa
tayari ameanza ujasiliamari wa kushona mashuka na kuyauza na hii nikutokana na
kupata pesa kwenye kikundi chao.
Licha ya kuanzisha ujasirilimali wa
kushona mashuka bado anakabiliwa na nchngamota ya vifaa kama vile chelehani ya
kushonea mashuka halii imekuwa ikipelekea kwenda kuazima kifaa hicha anapo pata
mteja.
“nimekuwa mbunifu wa kushona
mashuka lakini nimekuwa nikikosa
chelehani hali ambayo inanipelekea
kuazima kifaa hicho ninapo pata mtaja wa
shuka lakini nikiwa na kifaachangu
maisha yangu yatabalika kabisha kwana
mashuka nauza kwa bei nzuri tu” alisema Shamkubwa
Hadia Khamis Hilali ni mwanakikundi wa
tukiwezeshwa tunaweza yeye ananiambia
awali alikuwa mjariamali wa kusua
sua lakini baada ya kujiunga na na kikundi hicho faida nyinga amezipata
kutokana na kukopa nakuonngeza mtaji wake.
“Biashara yangu inazidi kukua siku
hadi siku na kutokana na kikikdi hiki
nimekuwa nikikopa na kurudisha mwanzo
lilikopo elfu hamsini Tshg (50,000) nikarudisha nasasa nimekopa Lakimoja na
Elfu Hamsini Tshg (150,000) pesahii nanunulia urembo na manukato nazunguka
mtaani kuuza na faida Napata alisema
Hadia
Kwa upanda wake Mohamed Salium Khamis
ni afisia mradi, mradi wa Kijaluba kutoka Chama cha wandishi wa Habari Tanzania TAmwa Zanzibar ofisi ya pemba amesema kuwa Mradi wa kijaluba
ni mradi jumuishi unaolenga kuwawezesha
watu wenye ulemavu kiuchu, kuwajengea uwezo watu wenye ulemavu kuhusu maisha
yao wenyewe pamoja na jamii.
Ameongeza kuwa katika kikondi kimoja
kina idadi ya watu 30 kati ya hao 20 ni watu wenye ulemavu na 10 niwatu wasio
na ulemavu wamekwa hao ili pale penye changamoto waweza kuwasaidia
Akitowa wito kwa vikundi hivyo ya
kuweka na kukopa amesema nivyema kufuata sharia zilizo wekwa huku mradi huo ukiangalia namna ya kuanzisha
biashara ya pamoja katika kila kikundi ambacho imejipangia kutekeleza
0 Comments