Na mwandishi wetu
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Siti Abass Ali amesema Idara hiyo ipo katika mchakato wa kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kwaajili ya kuifanyia maboresho sheria ya Mtoto namba sita (6) ya mwaka 2011 ili iendane na wakati uliyopo.
Akizungumza katika kikao cha ukusanyaji wa maoni
kilichowashirikisha wadau mbali mbali
wakiwemo viongozi wa dini, wanasheria, Jeshi la Polisi, n.k katika ukumbi wa Skuli ya Kidonge Chekundu
Unguja, jana alisema kutokana na vitendo vinavyojitokeza katika jamii,ikiwemo
ajira za utotoni hivyo, idara hiyo imelazimika kuipitia sheria hiyo nakuja na maamuzi
ya kuifanyia maboresha ili iendane na wakati .
“Kwa kweli Sheria hiyo imetusaidia sana na inaenaendelea kutusaidia,
imezungumza umuhimu wa mtoto kupata haki zake za msingi ikiwemo haki ya kupata
elimu, matibabu, chakula, malazi, malezi, pia imezungumzia jinsi gani mtoto
ataepukana na masauali ya udhalilishaji lakini baada ya kuipitia sheria hiyo
tumeona bora tuifanyie maboreshao ili iwe nzuri zaidi, pia tumeona ni ya muda kidogo, tangu ilipotungwa hadi leo
ni miaka kumi na mbili na vitendo vinaendelea
kujitokeza kama hili suali la ajira za utotoni ni changamoto kubwa” Alisema
Siti.
Alisema katika ukusanyajji wa maoni wameanza na makundi ya watoto
kupitia mabaraza ya watoto, viongozi wa dini, waandishi wa Habari, waratibu wa
kupinga vitendo vya ukatili na udhalilishaji, Wizara na Taasisi mbali mbali za
Umma na Binafsi, wakiwemo Wizara ya elimu, Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka
(DPP), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar (TAMWA-ZNZ), Jumuiya ya
Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), n.k.
Aidha Mkurugenzi Siti alifafanua kwamba umuhimu wa
marekebisho ya Sheria ya mtoto ni pamoja
na maendeleo ya sayansi na teknolojia
ambayo kimsingi yameongeza haja ya kuimarisha baadhi ya vipengele katika
sheria hiyo.
Naye Mkuu wa Divisheni ya Watoto wa Idara hiyo Mohammed Jabir
alisema kipengele namba 18 cha uanzishaji na uendeshaji wa mahakama ya Watoto
kimeeka wazi aina ya makosa na muda ambao mshatakiwa atapaswa kutumikia adhabu
au kifungo lakini adhabu hiyo sio kali hivyo ni wazi kwamba marekebisho yanahitajika katika kupengele hicho.
Pia alisema kipengeleza namba 12 kimezingatia majukumu ya
wazazi katika kuwasiamia Watoto ila bado wazazi hawakielewa na kukitumia
kinavyotakiwa katika kuleta mageuzi ya malezi bora kwa Watoto, hivyo kanuni
inahitajika ili iweze kutoa miongozo.
Kwa upande wa washiriki wa mkutano ambao ni wadau wa kupinga
Vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji wa kijinsia wamesema Sheria ya Mtoto namba
6 ya mwaka 2011 ni vyema ikatambua mgawanyo
wa haki za watoto kwa kuzingatia umri ili kulinda maslahi na ustawi wa
mtoto.
Akizungumza Hakimu dhamana Mkoa wa Kusini Unguja Khamis Rashid Khamis amesema ni wakati sahihi wa kueka sheria ambayo Itatoa muongozo wa kushughulikia watoto wenye umri wa chini ya miaka 14 na 16 na kuweka utaratibu wa kusikiliza kesi zao.
Idara ya Maeleleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea
na ukusanyaji wa maoni kwa kukutana na makundi mbali mbali katika jamii kwa lengo la kuipata maomi ili sheria mpya iwe
nzuri kwa na yenye maslah kwa mtoto.
0 Comments