Na Essau Kalubila.
‘’MIMI sasa sijioni mwanamke, najiona kama mwanamme mwenye uwezo mkubwa, ndio maneno ya mwanzo wa mlengwa kaya maskini Sakina Khamis Mbwana miaka (37), wa Shehia ya Tumbe Mashariki Pemba Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Nilipotaka kujua kwanini asijifananishe na mwanamke aliyepata
mafanikio, kwanza aliagusha kicheko na kusema, ameshahama kwenye uwanawake
kiuwezo, na sasa ni sawa na mwanamme.
Nilipomng’ang’ania sababu za kujifananisha na mwanamme, alisema
ilishazoeleka na kuaminika kuwa mwanamke hawezi kwa na mafanikio.
KABLA YA KUFIKIWA NA TASAF
Sakina kwa bahati mbaya, mwaka 2013 alifiliwa na mume wake,
aliyemuachia watoto sita, wakati huo wakiishi kwenye nyumba ya miti na makuti.
Matunzo ya watoto hao, anakumbuka kuyapata ndani mwezi mmoja,
baada ya kufiliwa na muumewake, ingawa kuanzia hapo, hakuna tena mchango hata
wa kupata majani ya chai kutoka kwenye familia.
Hadithi ikawa kwake yeye ni mgagaa na upwa hali ugali mkavu,
ingawa baadhi ya siku, akiukosa hata huo mkavu kula na watoto wake sita
mayatima.
Haki ya elimu kwa watoto, ilikuwa ni ya kusua sua, mara
wasimamishwe mara waruhusiwe kutokana na kutokuwa na uhakika wa mchango hata wa
shilingi 100.
Baada ya kuondokewa na mume wangu, kazi sasa ilikuwa ni kuuza
maandazi na maziwa eneo la soko la samaki Tumbe, ingawa kipato kilikuwa kidogo.
‘’Nikimaliza bidhaa hizi, ilikuwa faida haizidi shilingi 4000,
wakati ndani nina watoto sita, wanaohitaji mlo wa asubuhi pekee ni shilingi
6,000 kwa siku,’’anasema.
Alikuwa akimaliza bidhaa hiyo, miguu yake huelekea baharini
kuungana na wenzake, kwenye kilimo cha mwani ambapo kwa wakati huo, kilo mmoja
mkavu ni shilingi 700.
Hata alipojiunga kwenye kilimo cha mwani, anasema hakumbuki hata siku moja, watoto wake waliokula wakibakisha chakula kwenye dishi.
‘’Mimi ili nishibe vyema na watoto wangu, kuanzia asubuhi hadi
jioni, ilikuwa nahitaji shilingi 1,5000 kwa siku, ingawa nilikuwa natimiza
shilingi 5000,’’anasimulia.
Sakina hakumbuki watoto wake kuvaa nguo mpya hata siku za
sikukuu, na siku moja baada ya kukosa cha kuvaa, aliwatembeza watoto wake soko
la samaki Tumbe, baada ya kukosa hata nguo za mtumba.
‘’Wao hawakujua kwa sababu gani, tunakwenda kutembea sokoni,
badala ya eneo letu la kusherehekea sikukuu, lakini ilitokana na kukosa
nguo,’’anasilimulia.
Hakuwa na ndoto hata siku moja, kupata chakula cha kutosha,
kutimiza ada ya skuli ya watoto wake, au kufikia sikukuu wakavaa nguo za dukani
kama wenzao.
BAADA YA UJIO WA TASAF
Sakina anakiri kuwa, hakuamini alipoitwa na sheha wake, juu ya
kurodhesha majina ya watoto wake, na taarifa nyingine za maisha, akiona kama ni
mchezo.
Alikuwa na hakika kuwa, hakuna mpango wa kunusuru kaya maskini,
ambapo anaweza kulipwa fedha na pasi na kufanya kazi.
‘’Ukishakuwa na watoto yatima na hali yako ikiwa ya kinyonge,
atakuja huyu kukuandika, yule kukupiga picha na kisha mwisho wa siku, hakuna
jambo,’’anakumbuka.
Baada ya TASAF kuitia roho na kuitwa jina lake kwa ajili ya
kupokea, hakuamini moyo, macho na hisia zake kuwa amepata ruzuku hiyo.
‘’Siku ya mwanzo nilipokea shilingi 48,000 na nilielezwa ni kwa
ajili ya watoto, iwe katika elimu ya skuli au huduma za afya, na hapo ndio
nikaanza kuamini,’’anasema.
Sakina ambae yumo kwenye wale walengwa 14, 280 wa Pemba kuanzia
mwaka 2014 hadi mwaka 2019, anakumbuka fedha hizo, hakufanya kosa na
aliwanunulia vifaa vya elimu watoto wake.
Kuanzia hapo, watoto wake ilikuwa hawaendi skuli na sare mbovu,
viatu visivyofahamika na hakuna siku waliyorejeshwa kwa ukosefu wa michango wa
skuli.
Alidumu kwa miezi mitatu kupokea shilingi 48,000, ingawa baada
ya kukiuka masharti, alipokea ruzuku ya shilingi 36,000 kutoka TASAF.
MRADI WA KUKAANGA SAMAKI
‘’Nikiwa napokea shilingi 36,000 sasa nikamua niende
bandirini Tumbe, kununua samaki wa shilingi 10,000 kwa ajili kukukaanga na na
mafuta ya shilingi 200 na baada ya kuuza, nilipata faida ya shilingi
5000,’’anasema.
Mlengwa huyo, kazi hiyo ilimgia gegoni sawa sawa, na kuanzia
mwaka 2000, akawa ananunua samakini wa shilingi 45,000 hadi shilingi 50,000.
‘’Huku watoto wangu wakiwa wanakwenda skuli kama kawaida, na
biashara yangu iling’aa, na sasa hadi kufikia kujipatia faida ya shilingi
15,000 kwa siku kutoka ile shilingi 5000 ya zamani,’’anasema.
HAPA, baada ya kujikusanyia faida hadi kufikia shilingi 50,000
huku akiendelea kuwahudumia watoto wake sita mayatima, alizaa wazo la kuanzisha
genge.
Genge hili aliamua kuuza bidhaa kama tungule, bilingani, bizari,
nazi ingawa halikudumu, kutokana na kutokuwa na nafasi ya kuwepo nyumbani.
‘’Asubuhi nafuata samaki sokoni Tumbe, wakati huo huo natakiwa
nikafuatilie viungo vya mchuzi mjini, nikaona siwezi kujigawa, hivyo baada ya
muda genge niliacha,’’anasema.
Fedha alizoanzia genge na faida anayoendelea kuipata kwenye
samaki wa kukaanga, hadi inalifikia shilingi 20,000 sasa alizaa mradi mwengine.
Ingawa pembeni ya miradi hii, Sakina alikuwa akiendesha mradi
mwengine, wa kununua na kuuza sabuni za karafuu, akisema mwenyewe kwa ajili ya
chai ya watoto.
‘’Nilidumu nao kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu, lakini huu
ulikuwa ni baada ya saa za kazi, lakini hata navunja kisanduku mlikuwa na
shilingi 200,000,’’anasema.
MRADI WA NGUO ZA MITUMBA
Hapa, faida ya sabuni ya shilingi 200,000 ndio alioanza kununua
nguo za mitumba kutoka Kenya, ambapo alimtuma mtu aliyekuwa kuweko kwa shughuli
za uvuvi.
‘’Kwa sasa nimeshaolewa, na mume wangu alipofika Kenya wakati
anataka kurudini mwezi Disemba mwaka 2022, ndie niliemuagiza na sasa naendelea
na biashara hii hapa kwangu,’’anasema.
Mara ya kwanza, alipotuma shilingi 200,000 kwa bidhaa hiyo,
alijipatia faida ya shilingi 40,000 na sasa kwa mara ya pili, alituma tena
shilingi 400,000 ambapo hadi mwezi huu akiendelea kuuza.
Kwa
sasa anamiliki wastani wa shilingi milioni 1 kama mtaji, na hasa baada ya
kujiingiza kwenye kisanduku (kikoba), ambapo mwezi Machi mwaka 2023, alikopa
shilling 300,000.
MALENGO YAKE
Tayari ameshanunua kiwanja kutoka kwa familia, na hapo baadae
anajipanga kuanza ujenzi, ili aondokane na kodi ya mlango kwenye biashara yake.
Kwa sasa anaishi kwenye maisha ya ubinaadamu na furaha, na hasa
baada ya kuwaona watoto wake wanaendelea na masomo.
KATIBU WA SHEHA
Katibu wa sheha wa shehia ya Tumbe Mashariki,
Makame Hassan Makame, anasema wapo wananchi 20 waliomo kwenye mpango, ambao
sasa wamejiongeza.
Maana shehiani hapo, kati ya wananchi 7,675
waliofikiwa na mpango wa kunusuru kaya maskini walikuwa ni 231, ingawa kwa sasa
wanaoendelea ni 225, akiwemo Fatma Rubea Ali.
Wapo walioanzisha ushirika wa biashara kilimo
cha mboga, ufugaji vikundi vya kuweka na kukopa.
Lakini, akasema ipo miradi kadhaa ambayo
inawalenga jamii wote, kama vile ujenzi wa tuta la kinga maji, ambapo wakulima
zaidi ya 45, wamenufaika.
“Wakulima 45 walishayahama mashaba yao kwa
kuingia maji ya bahari, lakini TASAF ilianzisha mpango wa kujenga tatu la
kukinga maji, na sasa wakulima wamerudi,’’anasema.
Akaiomba TASAF, mara itakapomalizika mpango
huo kwa awamu ya kwanza, bado kwenye shehia yake, anao zaidi ya wanachi 200
wanaohitaji kunusuriwa.
MUUME WA SAKINA
Kwani hakupenda jina lake lichapishwe, ingawa
anasema mke wake sasa anamuona kama mfalme kwenye maisha yake.
‘’Hata namma ya kumshirikisha kwa kila jambo
langu la maisha, sasa najiona liko juu, maana amekuwa mtunza fedha na mtumiaji
mzuri,’’anasema.
Kwake sasa hana wasi wasi wa huduma za ndani,
maana mke wake amekuwa akitoa zaidi ya asilimia 60% ya kukamilisha huduma za
kila siku.
TASAF
Mratibu wa TASAF Pemba Mussa Said, anasema
wapo walengwa 14, 280 kwa Pemba, ambao wanaendelea kupata fedha za kunusuriwa
na umaskini.
Walengwa hao wapo kwenye shehia 78, ikiwemo ya
Tumbe Mashariki, ambapo tayari shilingi bilioni 14. 4 zimeshwafikia.
Mtu kama Fatma, ndio hasa malengo ya TASAF ya
kumtoa mwananchi katika unyonge, na kumleta kwenye taa, ili nae aishi maisha
mazuri.
“TASAF inaorodhesha ya zaidi ya walengwa
50,000 kutoka wastani wa walengwa 15 kila shehia, kati ya shehia 78, ambao
wamenzisha miradi ya kujikwamua.
“Mtu kama Fatma wa Tumbe, Amina wa Mgogoni,
Mfaki wa Kwale Gongo na Maryam wa Ukunjwi ambao hatuna shaka, hawawezi kurudi
tena kwenye umaskini mzito, wanafikia 50,000 kwa Pemba yote,’’anaeleza.
Mratibu Mussa anabainisha kuwa, kwa mwaka 2014
hadi 2015 walengwa hao wa kunusuru kaya maskini, waliibua miradi ya kijamii 41,
idadi iliongozeka mwaka uliofuata, kwa kufikia miradi 84.
Mwaka 2017 hadi mwaka 2018, walijukuta na
miradi mengine ya kijamii 21, inayuhusisha upandaji miti kama vile Makangale,
uazishwaji wa vitalu na ujenzi wa matuta ya kinga maji ya bahari Ndagoni,
Kiwani, Micheweni na Tumbe.
Achia mbali idadi ya watu 50,000 waliojiwekeza
wenyewe, vipo vikundi 942 vikizaa walengwa 12,000 vilivyoanzishwa, kuanzia
mwaka 2014 hadi sasa.
WANANCHI WA KAWAIDA
Fatma Hamad Mkandi, wa Tumbe anasema fedha
zilizoekezwa kunusuru kaya maskini, zimetumika vizuri kwa vile matunda
yanaoonekana.
Hassan Haji Omar, anasema kilichobakia sasa ni
tasisi nyingine kuvilea vikundi hivyo, ili walengwa wake wasirudi tena kwenye
umaskini.
‘’Kwetu sisi Sakina tumeshamuona kama mwanamke
mwenye uwezo mkubwa, sasa maana ruzuku ya TASAF aliitumia kama
inavyotakiwa,’’anasema.
Mwisho
0 Comments