Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi
Tanzania Awadh Juma Haji amewataka Askari kuendelea kudumisha nidhamu wanapokua
katika majukumu yao ya kila siku.
Ameyasema hayo huko katika chuo cha Polisi Ziwani
alipokua akiongea na Askari wanao shiriki mafunzo ya uongozi mdogo ngazi ya
sajenti alipokua akifungua mafunzo maalum yanayohusu kukabiliana na uhalifu
unaovuka mipaka na itakadi na misimamo mikali.
Pia amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha
linawejengea uwezo Askari wake katika kukubiliana na uhalifu na wahalifu na
wataendelea kushirikiana na jamii ili
kuhakikisha Tanzania inaendelea kua na Amani na utulivu.
0 Comments