HABARI MPYA

6/recent/ticker-posts

Mbunge Viti maalumu Mkoa wa Kusni Pemba Maryam Azani Mwinyi Atatua kikwazo cha maji Skuli zanufaika

VIFAA vyenye  thamani zaidi ya  milioni mbili  vimetolewa na mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Kusini Pemba Mhe Maryam Azani Mwinyi  ikiwemo mashine ya maji, matofauti na vifaa vyengine vya kujifunzia ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa vifaa muhimu kwa wanafunzi katika baadhi ya  skuli ya Mkoa huo

Mapema  mbunge huyo  amezi tembelea skuli  nne (4) Skuli ya Michakainia,Skuli ya  Maadnalizi Madungu Skuli ya sekondar Kilindi   kwa lengo la kujua changamoto zinazo patikana .

Akikabidhi  mashine ya Maji  , Matofali Elfu moja ,  mifuko  arobaini (40) ya Saruji , Manila ya kufundishia watoto na  ndoo za kuhifadhia uchafu  amesema kuwa  ataendeleza kutatua changamoto  na sasa ameanza katika sekta ya elimu

Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu  na Mafunzo ya Amali Pemba   Mohammed  Nassor  Salim amefurahisha na  mbunge kwa  kutatua kero  katika skuli hizo huku Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM  Mkoa wa Kusini Pemba  Mohamed Ali  amesema kuwa   chama kitaendelea  kuwahimiza  viongozi wake kutatua changamoto ndani ya jamii

Kwa upande wake  Abdalla  Omar Muya Mwenyekiti wa ujenzi Skuli ya sekondari Kilindi   amesema   msaada huo umefika muda mwafaka kwani utasaidia kumaliza changamoto ya vyumba vya kusomea


Post a Comment

0 Comments