IDARA ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Pemba inawashikilia vijana
wawili raia wa Comoro huku taratibu ya kuwarejesha nchini mwao zikichukuliwa
kwa ushirikiano wa Serikali ya Mkoa huo.
Vijana hao ni Jaffar Ibrahim Bakar (20) pamoja na Abdul Rauf
Dhwaafir Yussuf (20) walikokotwa na mawimbi ya bahari wakiwa na chombo chao cha
uvuvi aina na Fiber.
Mratibu Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Pemba
Seif Mohamed Seif amesema vijana hao wameokotwa katika bahari ya Kangagani
Wilaya ya Wete , baada ya kukaa baharini kwa muda wa siku kumi na mbili.
Kutokana na vijana hao kuzungumza lugha moja ya kikomoro, UGATv ililazimika kutumia lugha ya ishara ili kuwasilianao nao , ambapo wameshukuru ukarimu walioneshwa baada ya kuwasili Kisiwani Pemba.
#UGATvFurahaYako
0 Comments