ZOEZI LA kupiga
kura uchaguzi Mdogo wa nafasi ya Uwakilishi Jimbo la Pandani umemalizika na kutangazwa matokeo ambapo Prof Omary Fakih Hamad kutoka chama
cha ACT wazalendo ameibuka kidedea huku akiwashinda wangombea tisa walio shiriki katika uchaguzi mdogo jimbo
hilo.
Akitangaza matokeo ya
uchaguzi Khamis Abdalla Hassan afisa
uchanguzi mkoa wa kaskazini pemba amesema kuwa Omar Fakih Hamad ameshinda kwa
kura 2361 sawa na sailimia 52.5 huku
akifatiwa na Mgombea kupitia chama cha ccm Mohamed Juma Ali
alie pata kura 1934 sawa na aslimia 43.
Kwa upande wao walio
shindwa katika uchaguzi huo wameishukuru
tume ya uchaguzi kwa kwendesha zoezi
hilo kwa huru na haki na kuwataka wanchi kushurikiana na mshindi alie
patikana
Jimbo la Mpandani linafanya Uchaguzi wa Mwakilishi kufuatia
kifo cha aliyekuwa Mwakilishi Mteule wa Jimbo hilo Abubakar Khamis Bakari
kupitia Chama cha ACT Wazalendo kufariki dunia, usiku wa kuamkia Novemba 11,
2020.
#UGATvFurahaYako
1 Comments
Karibu sana sisi ni Furaha Yako
ReplyDelete