Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Mahamoud Banga amewaonya madereva Bajaji mkoani humo kuondoa mara moja taa kali ambazo zimefungwa kwenye vyombo vyao kwani taa hizo zimekuwa zikisababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara ikiwemo ajali.
TAZAMA VIDEO: VIDEO LINK
Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na madereva hao kufuatia oparesheni ya kukamata vyombo vinavyofanya shughuli bila kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwemo ufungaji wa taa kali, namba za usajili, bima na leseni kwa madereva hao.
0 Comments