+
NA Masanja Mabula -PEMBA
NI takribani robo karne imepita tangu sheria ya Habari Zanzibar imefanyiwe mabadiliko ambayo hata hivyo bado hayajaleta suluhisho la changamoto zinazawakabili wandihsi wa habari
Kwa kipindi chote
hicho wadau wa habari wakiwemo wandishi wa habari wamekuwa wakipiga chapuo
kuomba sheria ambazo ni kandamizi ziweze kuondoshwa ili kutoa uhuru wa
wanandishi na wadau wa habari kutumia vyema tasnia hiyo kwa lengo la kuleta
mabadiliko chanya.
Kubadilishwa au
kufanyia marekebisho sheria kandamizi ikiwemo ile ya Usajili na Uwakala wa
Habari, Magezeti na Vitabu No/1988 ambayo ilifanyiwa marekebisho 1997 itatoa
fursa na mawanda mapana kwa wadau na wandishi wa habari kutimiza malengo na
wajibu kihabari.
Kupitia kifungu cha
30 cha sheria hii kimetoa mamlaka makubwa mno kwa Waziri wa Habari kuweza
kuchukua maamuzi ya kukifungia na kusitisha kazi za chombo cha habari pasi na
kuhitaji ushauri kutoka mamlaka nyengine.
Makala haya
imefanya mahojiano na baadhi ya wandishi wa habari nguli , weledi na waboboezi
wa tasnia ya habari Kisiwani Pemba ambao wametoa maoni yao juu ya sheria hii
ambayo wamiitaja kuwa ni kikwazo cha maendeleo na uhuru wa wandishi wa habari.
Ali Massoud Kombo
Meneja wa Kituo cha Redio Jamii Micheweni amebainisha kwamba Sheria hii sio tu
kuwa nikandamizi bali pia inaviza maendeleo ya habari nchini.
Katika mahojiano na
Makala haya Ali Masoud Kombo anasema mabadiliko ya baadhi ya sheria ikiwemo
sheria hii Usajili na Uwakala wa Habari, Magezeti na Vitabu No/1988 ambayo
ilifanyiwa marekebisho 1997 ili iendane na maendeleo ya tasnia ya habari.
“Kwa sasa sisi
wasimamizi wa vituo vya Redio za Kijamii kila siku tunaamka na kusikiliza
vyombo vya habari kujua Waziri kama hajachukua maamuzi ya kusimamisha matangazo
au kufungia vituo vyetu, yaani siku zote huwa sina amani huwa na hofu, kwani
huwezi jua Waziri atamka vipi siku hiyo”alisisitiza.
Picha ni Essau Simon Kalukubila mmiliki wa UGA MEDIA ambae pia ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Jamii Micheweni.
Naye Essau Simon
Kalukubila Mmiliki wa UGA MEDIA,amesema sheria hii ni kongwe na ambayo
ilitungwa kulingana na mahitaji ya wakati huo,kwa sasa inahitaji kufutwa baadhi
ya vifungu ambavyo vinaonekana kuwa ni kandamizi.
“Tangu niingie
kwenye tasnia ya habari, wandishi na wadau wa habari wanaendelea kupaza sauti
zao kuziomba mamlaka husika kuzifanyia marekebisho badhi ya sheria
ikiwemo hii Usajili na Uwakala wa Habari, Magezeti na Vitabu No/1988 lakini
zimeshindwa kufanyiwa marekebisho au sijui hawa wahusika wanainterest
nazo”alihoji.
Naye Ali Khatib
Chwaya Mwandishi wa Habari Mkongwe Kisiwani Pemba anasema mabadiliko
yanahitajika kwani wakati sheria hii inatungwa ilikuwa sahihi kulingana na
wakati huo kwa kuwa kulikuwa na vyombo vichache vya habari.
"Nyinyi
wandishi wa habari mnaochipukia endeleeni kupaza sauti kuomba hichi kifungu
ambacho kinaviza uhuru wa habari kiondoshwe ,jambo ambalo pia
litawafanya muwe huru kutekeleza majukumu ya kuihabarisha jamii”alishauri.
Akizungumza na
wandishi wa habari kwenye mafunzo ya Sheria ya Habari Mmiliki wa Blog ya Pemba
Today Haji Nassor Mohammed amewataka kushirikiana katika kudai marekebisho ya
sheria kandamizi zinazobinya uhuru wa wandishi.
Amesema zipo sheria
nyingi ambazo zinaonekana kuwa shubili (chungu) kwa tasnia ya habari ikiwemo
hii inayompa mamlaka waziri wa kufungia na kusitiza utoaji wa huduma
(Kuhabarisha) kwa chombo cha habari.
“Mapambano haya
tutashinda iwapo kila mmoja kwa kutumia chombo chake ataandika na kutangaza
taarifa zinazotaka marekebisho ya sheria hii, itafika wakati wakubali na
kuzirekebisha kama sio kuziondoa kabisa.
Mwandishi wa Makala
haya binafsi nikiri kwamba mmoja wa wandishi wa habari Kisiwani Pemba ambaye
anafaa kuungwa na mkono, ni Haji Nassor Mohammed ambaye amekuwa ni mfano wa
kuigwa katika mapambano haya ya marekebisho ya sheria kandamizi.
Moja ya Makala yake
na hapa na nukuu “Kwa mfano, kifungu cha 27(2) cha Sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari,
Magazeti na Vitabu Na. 5 ya 1988,Kwa muktadha huo, kifungu cha maneno
yaliyotumika yana utata ndani yake, maana hayaeleweki sawasawa kwa sababu
kimekusanya maneno mengi na tata, yasiyofahamika”mwisho wa kunukuua
Kwa upande wake
Hawra Shamte, mwandishi wa habari Mkongwe Visiwani hapa, akitoa mafunzo kwa
wandishi wa habari katika Ofisi za Tamwa Pemba alisema kifungu hicho kinampa
mamlaka waziri kukifungia chombo cha habari pindi akiona yeye
“Hichi kifungu
kinahitaji kuondohwa kwani kinakandamiza uhuru wa habari, kwani ni vigumu
kuweza kubaini dhana na shuku, hivyo tunashauri kiondoshwe,” alisema.
Kwa upande wa wadau
wa habari na kilio chao ni kwa sheria hii kwani wanasema ikiachwa iendelee
kutumia inaweza kusababisha umaskini kwa jamii.
Mohammed Suleiman
(Babu Eddy) mmiliki wa Rada Online TV, amesema kitendo cha waziri kupewa
mamlaka makubwa na sheria ya kuweza kukifungia chombo chochote cha habari
kinaweza kuwa ni sababu ya umaskini.
“Vijana wengi
wamewekeza kwenye mitandao ya kijamii, hivyo waziri akiamka na kutoa maamuzi ya
kufungia chombo cha habari itachangia umaskini kwani chombo kinategemewa na
baadhi ya vijana kuendesha maisha yao”alisema.
Hata hivyo wandishi
wa wadau wa habari wameshauri na kutoa mapembezo yafuatayo;-
Kabla ya waziri
kuchukua maamuzi ya kukifungia chombo cha habari , anapaswa kushauriana na
wadau wa habari ikiwemo BARAZA LA HABARI TANZANIA –MCT-pamoja na wadau wengine
wa habari wakiwemo Vilabu vya wandishi wa habari na TAMWA.
Kuundwe bodi ambayo
itakuwa na jukumu la kusimamia na kuratibu mwenendo wa vyombo vya habari.

0 Comments