HABARI MPYA

6/recent/ticker-posts

MFAHAMU IMANE DUWE MWANAMKE ALIELETA MABADILIKO KATIKA MASHINDANO YA MAPINDUZI CUP ZANZIBAR


 Kwa muda mrefu tumezoea kuona sekta ya michezo mara nyingi ni ya wanaume kwa tunaamini kuwa ndio weledi na wenye uwezo mkubwa wa kusimama kwenye michezo jambo ambalo kwa sasa tumeona mabadiliko makubwa ambayo yamefanywa na wanawake wengi katika kuingi kwenye sekta hiyo, mfano Mzuri tukianzia kwenye serikali ya awamu ya 8 kwa kuwaamini wanawake na kuwaweka kwenye usimamizi wa wizara ya inayohusiana na michezo.

Mbali na hayo wanawake wamekuwa na nafasi pana katika nafasi hiyo kwani licha ya viongozi, zipo na timu mbalimbali za wanawake nchini Tanzania, lakini pia wapo waamuzi wanawake ambao kwa sasa wamepata leseni na kuchezesha michuano mbalimbali Nchini.

Mnamo Januari 28, 2022, Shirikisho la soka Afrika (CAF) limewateua marefa wa kike wa Tanzania, Florentina Zabron, Janeth Balama, Helen Mduma na Tatu Malogo kuchezesha mechi ya kufuzu kombe la dunia kwa wasichana U17 baina ya Djibouti na Burundi kati ya machi 4 na 6 jijini Bujumbura.

Tukigeukia katika Historia ya kombe la Dunia kamati ya FIFA iliteua marefa watatu wa kike kwa mara ya kwanza katika historia kuamua mechi katika kombe la dunia mmoja wa marefa hao ni Salima Mukansanga Raia wa Rwanda ambaye aling'aa katika mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) ambapo jumla ya marefa 36, marefa wasaidizi 69 na marefa wasaidizi wa video (VAR) 24 walikuwepo nchini Qatar kuamua michuano ya kombe hilo.

Mwengine ni Stephanie Frappart mfaransa mwenye umri wa miaka 38 amekuwa na taaluma nzuri ya urefa, akiwa mwanamke wa kwanza kuwa refa wa kati katika mechi ya kombe la klabu Bingwa Ulaya.

Na Yoshimi Yamashita raia wa Japan ambaye alikuwa ni refa wa kwanza mwanamke kusimamia mechi ya kombe la klabu bingwa barani asia mapema mwaka huu.

Kando na marefa hao watatu, kamati ya FiFa pia iliwateua wanawake watatu kuhudumu kama marefa wasaidizi katika mashindano hayo ambao ni pamoja na Neuza Back kutoka Brazil, Raia wa Marekani Kathryn Nesbitt na mwenzake Karen Diaz Medina kutoka taifa la Mexico.

Leo nataka kunena mambo kadhaa juu ya mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayoendelea visiwani Zanzibar na namna ambavyo ni fahari katika macho ya watazamaji Tanzania na nje ya mipaka yake.

Malengo ya kuanzishwa kwa michuano ya kombe la Mapinduzi pasi na shaka ni mengi ikiwa ni pamoja na kusherehesha maadhimisho ya mapinduzi matukufu ya zanzibar january 12, 1964 ambapo fainali ya michuano hiyo hufanyika siku moja baada ya kilele cha maadhimisho ya mapinduzi.

Mashindano haya pia yalianzishwa kama sehemu ya kuibua na kukuza michezo visiwani Zanzibar. Licha ya yote hayo lakini imekuwa ni nadra sana kwenye mashindano haya kuona yanaendeshwa na mwanammke kwani tokea kuanzishwa kwake mwaka 1998 ni misimu miwili tu ndio ambayo tumeona ikiongozwa na wanawake.

leo wacha tuuangazie msimu wa 2022 ambao umeongozwa na Imane Duwe namna ulivyokuwa pamoja na kubadilisha ubora wa mashindao hayo katika mwaka huo.

Tukumbuke kuwa Imane Duwe ni mwanammke wa pili kufanikiwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi kwenye historia ya Kombe la Mapinduzi akitanguliwa na Sharifa Khamis Salim, kwa Muda mrefu Imane alipata nafasi ya kuwa mjumbe tu kwenye kamati ya Kombe la Mapinduzi lakini kwenye msimu ambao aliuongoza hakutaka kuendeleza walipoishia wengine bali alikuja na mikakati yake mipya yaliyoongeza ubora, ushindani na kukuwa zaidi kwa kombe hili la mapinduzi.

Katika mazungumzo yangu na Mwenyekiti Imane Duwe ni vitu vingi aliweza kuviboresha licha ya kuanza kwa mfumo mpya wa kutoupewa pesa kwa serikali jambo lililowapa changamoto kubwa katika kutafuta wadhamini ili kuweza kuziendesha timu kubwa zinazoshiriki.

Kwa Mujibu wa Imane Duwe katika vitu alivyoviengeza ni pamoja na burudani wakati wa mapumziko wa mechi pamoja na kuwaweka sehemu nzuri viongozi wa timu zinazoshiriki mapinduzi, pamoja na kuwawekea malipo, usafiri na vyumba maalumu kwa waamuzi ili na wao waendane na hadhi ya mashindano hayo.

Katika mwaka huo pia jambo pekee kubwa alilolifanya ni pamoja na kuweka tiketi kwa ajili ya watoto jambo lililoruhusu watoto wengi kuangalia mashindano hayo pamoja na kufanikiwa kuanzisha mfumo wa utoaji wa kombe uwanjani tofauti na jukwaa kuu kama ilivyozoeleka hapo awali.

Changamoto kubwa kwenye mashindano haya ni Timu kubwa Simba na Yanga namna ya kuzihudumia kuanza usafiri makaazi na malazi jambo ambalo lilitupa changamoto kubwa sana lakini tulipambana na tuliweza” alisema Imane Duwe.

Aidha Mwenyekiti Imane aliongeza kuwa katika kitu ambacho daima hataacha kujivunia katika uongozi wake ni kuweza kurejesha fedha serikalini kipindi ambacho walitakiwa wajitegemee wenyewe.

 

Katika moja miongoni mwa majukumu ya kamati ya Kombe la Mapinduzi ni kiuhakikisha mashindano hayo yanachezeshwa kwa haki na kuwa sehemu ya kukuza vipaji vya soka pamoja na kuwapa fursa wachezaji wazawa kuonekanwa kimataifa.

Baadhi ya waliokuwa wajumbe wa kamati hiyo walielezea kuwa usimamizi na mikakati imara ya wa kamati ndio ambayo ilipelekea mashindano kuwa ya kipekee walieleza kuwa katika jambo lililowasukuma kwa kiasi kikubwa kwenye mafanikio ni ushirikiano pamoja kuanzisha mikakati ya kuboresha miundombinu yote inayohusu mshindano hayo ikiwemo kurekebisha maeneo ya viwanja vilivyokuwa vikitumika hasa Uwanja wa Amani ambao ndio uwanja mama kwenye mashindano hayo.

Aidha waliongeza kuwa msimamo imara wa mwenyekiti wao katika kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa kikamilifu katika mashindano hayo ikiwemo vikao vya maandalizi kwa timu, kuwaandalia viwanja vya mazoezi pamoja na kusimamia ratiba za timu hizo na kuhakikisha hakutokei kitu kitakachokwamisha ratiba hizo.

Tukirudi katika Hotuba Ya Bajeti Ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni Na Michezo iliyowasilishwa na Mheshimiwa Tabia Maulid Mwita Kuhusu Makadirio Ya Mapato Na Matumizi Ya Fedha Kwa Mwaka 2023/2024 katika kipengele cha Programu ndogo ya Uendelezaji na Ukuzaji wa Michezo inayotekelezwa na Idara ya Michezo na Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar ambayo iliidhinishiwa jumla ya shilingi 7,483,200,000 ambapo katika kuhakikisha programu hiyo inatekelezwa kwa ufanisi miongoni mwa shughuli zilizopangwa ni kutekelezwa na kuandaa mashindano ya kombe la Mapinduzi CUP.

Akizungumza kwa niaba ya wasemaji wa timu zilizoshiriki Kombe la Mapinduzi mwaka 2022 Khamis Haji Khamis msemaji wa timu ya KMKM walielezea kuwa mwaka wa huo ulikuwa na hamasa kubwa ya mashabiki pamoja na ushindani kwa timu zilizoshiriki lakini pia utaratibu mzuri wa upangaji wa Ratiba kwa vilabu vilivyoshiriki mashindano hayo jambo lililotoa muda mzuri kwa vilabu hivyo kujiandaa.

Simba Sports Ndio iliyoibuka kidedea katika mashindano baada ya kuichapa Azam Fc goli 1-0, kujinyakulia kombe pamoja na kitita cha Shilingi Milioni 25 za Kitanzania.

MWISHO..

Post a Comment

0 Comments