HABARI MPYA

6/recent/ticker-posts

MFAHAMU BIBI MWENYE NDOTO ZA KUFUNGUA DUKA LA GUO, KUWASOMESHA WAJUKUU HADI CHUO KIKUU

 Na Essau Kalukubila.

KHADIJA Ali Mohamed 45, wa Chimba Micheweni Mkoa wa Kaskazini  Pemba, sasa ana mtaji wa zaidi ya shilingi 700,000, anayo matofali 500 na kiwanja.

Mpango wake huo, ni zao la ule mpango wa kunusuru kaya maskini, unaosimamiwa na TASAF tokea mwaka 2014, ambapo kila baada ya miezi mwili, hujipatia ruzuku kati ya shilingi 30,000 hadi shilingi 44,000.

Ijapokuwa mlengwa mmoja na mwengine hutofautiana upatikanaji wa ruzuku hiyo, lakini zipo fedha za msingi (lazima) ambapo kila mlengwa, hupata shilling 20,000.

akizungumuza na mwanashi wa habari hizi Khadija anakiri kuwa, mpango ya kuingizwa kwenye utaratibu wa TASAF, kwake ulikuwa sahihi, kwani hapo kabla, alikuwa akiishi kiwango cha shilingi 5000 kwa mwezi.

KABLA YA KUINGIA TASAF

Kwake mlo wa siku, hakuwa na hakika nao, kutokana na kutokuwa na hata njia moja, ya uhakika ya kujiingizia kipato, licha ya kutegemewa na watoto wake wanne wakati huo.

“Asubuhi nikiamka, ilikuwa najiuliza kwanza nisuke makuti ya mnazi niuze nipate kiamsha kinywa, au niende shambani kulima muhogo, jambo hilo lililoniweka roho juu,’’anasimulia.

Kwa wakati huo, huku akipambana na maisha bila ya mafanikio, alikuwa akiishi kwenye nyumba ya tope, iliyoezekwa makuti ya mnazi, iliyokuwa na mlango mmoja wa bao moja lisilo rasmi.

Huduma za watoto alioachiwa na mume wake, zilikuwa za omba omba tena bila ya mafanikio, na wakati mwengine kujifungia ndani, pasi na kifungua kinywa.

Suala la watoto wake kwenda skuli, kutasaka haki ya elimu na madrssa, lilikuwa la kubahatisha, kutokana na maisha yake kuzungurukwa na changamoto hasa za kipato.

“Ilikuwa nikihitaji shilingi 1000, kama ninae hitajia shilingi 500,000 hapo ni kusuka makuti, ili kutatua changamoto zangu na watoto wangu za kimaisha,’’anasimulia.

Anakumba vyema, wakati anapodaiwa michango ya familia, iwe ya kufiwa, harusi na ugonjwa na kuieleza familia juu ya kukosa kwake, hakuwa akifahamika juu ya hilo.

Hakuna hata siku moja, aliyoota ndoto ya kuondokana na hali hiyo ngumu au kuishi kwenye nyumba ya kisasa, kama walivyo wetu wengine.

Hii ni kutokana na mipango yake ya kimaisha, hasa ya kutafuta fedha, haikuwa na mwelekeo, achia mbali mlo wa kila siku ambao ni wa lazima.

BAADA YA TASAF

Kuanzia mwaka 2014, anasema baada ya kuitwa na kuhojiwa na uongozi wa shehia ya Chimba wilaya ya Micheweni, hakuamini alichoelezwa.

“Si unajua kila mmoja atapita, huyu atakuhoji, huyu atakuandika, yule atakupiga picha na mwengine hadi kuchora ramani ya unapoishi, lakini mwisho wa siku, hakuna jambo,’’anasema.

Hata kwa upande wa mpango huo wa kunusuru kaya maskini, rasmi alijenga roho ya tamaa na furaha, baada ya mara ya kwanza kupokea ruzuku ya shilingi 44,000.

“Fedha hizo, kwanza niliwanunulia watoto wangu vifaa vyote vya skuli na madrassa, na kisha saa siku hiyo 7:00 mchana nilipika chakula kizuri na samaki mnene,’’anahadithia.

Miaka nenda miaka rudi, Khadija sasa akawa anaendelea kupokea fedha hizo, kati ya shilingi 30,000 hadi shilingi 80,000 wakati mwengine, hutegemeana uwepo wa ajira za muda.

Baada ya miezi minane, kuona mpango huo umedumu mikononi mwake, alianza mikakati ya kuziendeleza fedha hizo, huku moja akipiga hesabu, namna ambavyo ataanzisha ujenzi wa nyumba ya kisasa.


‘’Hapo baada ya kuzaa wazo la ujenzi, nikaanza kuzigawa fedha nusu nakula na kuhudumia watoto, na nyingne nafundika (akiba) pembeni hadi zikatimia shilingi 150,000,’’anasema.

Hapo sasa aliwaita watoto wake, na hasa baada ya familia kumkubalia ombi la kununua kiwanja cha ujenzi wa nyumba.

‘’Kiwanja niliuzia shilingi 300,000 na mimi nikatoa shilingi 150,000 na watoto wangu wakanisaidia kima kama hicho, na sasa nn ummiliki rasmi,’’anasimulia.

 Huku watoto wakienda skuli, bila ya shaka na kazi zake nyingine aliendelea zao kama vile kilimo, kuuza nazi naususi wa makuti ya mnazi, wazo sasa likawa ni kuanzisha biashara.

“Nilimshauri mtoto wangu anaekwenda kwa uvuvi nchini Kenya, aninunulie nguo za mtumba, na kisha azipeleka huko, maana biashara hiyo inakwenda,’’anasema.

Kwa hatua za mwanzo, alinunua mitumba ya shilingi 150,000 na baada ya kuuza, alipata faida ya shilingi 50,000 na kuingia ari mara mbili.

Walishasema wahenga kuwa, utamu wa sukari huja mwisho, nae sasa baada ya kupata faida hiyo ya awali, mara ya pili alituma mzigo wa shilingi 250,000.

Kwa awamu ya pili, biashara haikuwa mzuri, ingawa mlengwa huyo wa kaya maskini, alijipatia faida ya shilingi 30,000 ambapo mara ya tatu, alituma tena mzigo wa shilingi 300,000.


“Kwa sasa sipungui wastani wa mtaji wa shilingi 700,000 kama mtaji ambapo naendelea na biashara yangu hiyo, na tayari pia nimeshanunua matofali 500,’’anaeleza.

Kumbe wakati huu akiendelea na ujasirimali wake wa nguo za mitumba, akiwa anamilki kiwanja cha kujenga nyumba na matofali yake 500, pia ni mkulimwa wa mboga.

“Nataka nyumba yangu iwe na vyumba vinne na vyoo viwili, ili sasa familia yangu na hasa wajukuu, wapate utulivu zaidi kupitia matunda haya ya TASAF,’’anasema.

Kwenye kilimo cha mboga, alikojiegesha na wenzake wa mpango wa kunusuru kaya maskini, hujipatia faida kati ya shilingi 30,000 hadi shilingi 40,000 kwa mwezi hutegemea na soko lilivyoamka.

Kwenye mfuko wa ushirika wao wa kuweka na kukopa, mlengwa huyo anatimiza shilingi 350,000 kama mtaji wake binafsi, ambpo wakati mwengine, hukopa na kulipa.

‘’Unajua TASAF ilitutaka tuhakikisha fedha za ruzuku wanazotupa zisiishie kwenye dishi pekee, bali tuziekeze ili zizae, na hili nalifanya kwa vitendo,’’anasema.

Kwake yeye anaamani siku moja TASAF itakapoondoka mikononi mwake, na kwenda kwa wenzake, awe na jambo la kujisifia kimaisha.

MALENGO YAKE BAABADAE

Moja ni kuwa na mlango wa wa duka, ambapo hapo sasa anatarajia kuwa na biashara ya nguo, zisizokuwa za mitumba, na kuhakikisha wajukuu anaowalea, anasomesha hadi chuo kikuu.

Kwa sasa mlengwa huyo wa kaya maskini, anaendelea na shughuli zake kama kilimo, ususi wa makuti akiongeza na ujasriamali wa nguo za maitumba.

SHEHA 

Sheha wa shehia ya Chimba wilaya ya Micheweni Saleh Salim Khamis, anasema shehia yake, inawananchi 168 waliomo kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini, kati ya wananchi 4,215.

Anacho cha kujivunia ndani ya shehia yake, ikiwemo walengwa hao kuanzisha vikundi saba vya ushirika, vyenye wanachama zaidi ya 150.

“Kwenye shehia yangu, pamoja na mlengwa mmoja mmoja kujiajiri, ipo miradi ya mikubwa, ambayo wananchi wote wamenufaika nayo,’’anasema.

Hata hivyo Katibu wa sheha wa shehia hiyo Omar Salim Hamad, anasema TASAF, imeikomboa shehia yao kwa kuwepo vikundi ambavyo kwa njia ama nyingine, wanachama wake wameshaondokana na umaskini wa kipato.


‘’Mfano ushirika wa maskini hajengi, wanaolima mboga na ufugaji wa kuku, lako jicho ni ushirika wa ufugaji, uwekaji hisa na kilimo cha mboga na kukusanya walengwa 20,’’anasimulia.

TASAF

Mratibu wa TASAF Pemba Mussa Said, anasema wapo walengwa 14,280 kwa Pemba ambao wanaendelea kupata fedha za kunusuriwa na umaskini.

Walengwa hao wapo kwenye shehia 78, ikiwemo za Tumbe Mashariki, Chimba, Makangale, Kiwani, Ndagoni, Ukunjwi na Fundo.

Ambapo tayari TASAF Pemba, imestumia shilingi bilioni 14.4 kwa ajili ya kuwapa ruzuku walengwa hao, fedha za kazi na zile za msingi, pamoja na za masharti.

Tayari kila shehia, kati ya hizo 78, zimesafikiwa na wastani wa zaidi ya shilingi milioni 230, ambapo kwenye walengwa wote 14,280 wa Pemba, na kila mmoja ameshasaini shilingi milioni 274.619, ingawa inategemeana na eneo husika.

Mratibu wa TASAF, alimtolea mfano wa kuigwa mlengwa Khadija wa Chimba, Amina wa Mgogoni na mwenzake Mfaki kuwa wameyatekeleza kwa vitendo malengo hasa ya mpango huo.

‘’Wenzetu kama hawa ambao wapo zaidi ya 50,000 kwa Pemba nzima, wamekwenda sambamba hasa na malengo na mwelekeo wa TASAF, wa kumtoa mwananchi katika unyonge hasa wa kipato,’’anasema.

Jengine ambalo ni jema, ni kwa walengwa hao kuanzia mwaka   2014 hadi mwaka 2018 kuibua miradi ya jamii 146, kwa ajili ya wananchi, kama vile ufufuaji wa mito ya asili na ujenzi wa daraja ndogo.

‘’Mfano wa miradi hii hata Makangale upo wa upandaji miti, ujenzi wa matuta ya kuzuilia maji ya chumvi, mfano Ndagoni, Tumbe na Micheweni,’’anafafanua Mratib wa TASAF Pemba.

 Achia mbali idadi ya watu 50,000 waliojiwekeza wenyewe, vipo vikundi 942 vikizaa walengwa 12,000 vilivyoanzishwa, kuanzia mwaka 2014 hadi sasa, ingawa vilivyosajiliwa ni 700.

SERIKALI KUU  

Makamu wa Pili wa rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdall, anasema lengo la TASAF ni kuona mwananchi mmoja mmoja anaondoka kwenye wingu la umaskini hasa wa kipato.

Anasema, fedha zilizotumiwa na TASAF Pemba pekee wastani wa shilingi bilioni 14.4 lazima zizae matunda, ili wananchi waweza kuongeza pato lao.

Post a Comment

0 Comments