MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Maryam Azan Mwanyi ameongoza zoezi la uchangiaji damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa ambao wapo katika hosipital za wilaya mbili za chake chake na Wete kutokana na kuwepo kwa madaktari bingwa wa upasuaji katika vituo hivyo.
Akizungumuza na Wasafi fm mara baada ya kamaliza kuchangia damu Mh Maryam amesema kuwa ameamua kuendesha zoezi hilo kwa lengo la kuokoa maisha ya wanawake wangi ambao wapo katika Hospital za Pemba ambao wamekuwa wakipoteza maisha kwa kukosa huduma ya damu.
Kwaupande wao wananchi wameonesha kufurahishwa na kitendo hicho cha mbunge kuendesha zoezi la uchangiaji damu kwa jamii imekuwa bado haina mwamuko wa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa.
Kwaupande wake afisa mdhamini Wizara ya Afya Usitawi wa Jamii Jinsia Wazee na Watoto Pemba Yakuob Moh’d Shoka ameitaka jamii kuwa na utalatibu wa kuchangia damu ili kusidia na kuokoa maisha ya mama na mtoto pamoja na wagonjwa wengine .
0 Comments