Mbunge
wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amefunguka na kusema kuwa picha za darasa
ambalo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zilikuwa zikimsumbua kiasi
cha kuamua kuchukua jukumu la kufanya mabadiliko katika darasa hilo
mpaka sasa kuwa shule.
Nape
Nnauye amesema kuwa baada ya yeye kuwa mbunge mwezi mmoja au miwili
baadae zilianza kusambazwa picha za wanafunzi wakiwa wanasoma chini ya
darasa hilo ambalo hali yake ilikuwa mbaya kwani lilikuwa ni darasa la
miti tu huku wanafunzi wakikaa kwenye miti pia.
"Nikiri
kwamba msukumo wa ile picha kwenye mtandao wa jamii ulikuwa na mguso wa
pekee yake kuliko ningesimuliwa kawaida, baada ya kuona ile picha
imesambaa na anayesemwa ni mimi nikaaamua kufunga safari nikaja nikasema
jamanii hii ni aibu kwetu tumesemwa kwamba vijana wetu wanasoma kwenye
darasa bovu kwa hiyo nikaamua na kukaa pamoja na wenzangu tukaweka
mkakati.
"Nikaleta
mifuko ya cement na kuanza kazi ya kufyatua tofali tukaanza na madarasa
machache hivyo tulipigana kutoka kwenye hili darasa kwenda kwenye hayo
madarasa mengine ambayo sasa yamefika manne na tunaendelea kwani
tunataka iwe shule yenye madarasa ya kutosha na ikiwezekana na nyumba za
walimu" alisema Nape Nnauye
0 Comments