HABARI MPYA

6/recent/ticker-posts

Yanga yaifumua African Lyon 3-0

Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara, Yanga wameanza vyema kutetea taji lao baada ya kuilaza African Lyon mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Taifa.

Yanga inayoonekana kuiva hasa, pengine kutokana na kukomazwa na mikiki ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika, ilianza kuandika bao la kwanza kupitia kwa Deus Kaseke baada ya winga huyo kuvunja mtego wa kuotea, akiuwahi mpira wa Thaban Kamusoko na kuukwamisha wavuni kiurahisi.

African Lyon ilionekana kuwa kimya muda mwingi wa mchezo, ilipachikwa mabao mengine mawili kipindi cha pili.

Simon Msuva alifunga bao murua akimpiga kanzu mlinda mlango baada ya kuwahi pasi ndefu ya Thaban Kamusoko, kiungo nayeonekana kuwa kwenye kiwango cha juu karibu kila mchezo anaocheza.

Juma Mahadhi ambaye aliingia dakika 15 kabla ya mpambano kumalizika akichukua nafasi ya Simon Msuva, aliifungia Yanga bao la tatu kwenye dakika za majeruhi.

Licha ya kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga kipindi cha pili, washambuliaji wa African Lyon wakiongozwa na Okello walikosa mbinu ya kuipenya safu ya ulinzi ya Yanga iliyokuwa chini ya Vicent Boussou na Vicent Andrew 'Dante'.

Post a Comment

0 Comments